Na. Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

 
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana na kubadilishana uzoefu na nchi ya Qatar kukuza sekta ya fedha pamoja na utafiti, uchimbaji na uendelezaji wa gesi asilia ili sekta hizo ziweze kuchangia zaidi ukuaji wa uchumi wa nchi.

Mhe. Balozi Omar amesema hayo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea ujumbe maalumu kutoka nchi hiyo na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Mhe. Fahad Rashid Al-Marekhi.

Alisema kuwa Qatar ina uzoefu mkubwa katika sekta ya utafutaji, uchimbaji na uendelezaji wa gesi asilia eneo ambalo Tanzania inaweza kujengewa uwezo zaidi.

“Tunafahamu kuwa Tanzania tumegundua gesi asilia na tayari kuna maeneo ambayo tunaendelea kuichimba na kuitumia kwa hiyo tunaweza kubadilishana uzoefu katika eneo la utafutaji na namna walivyoweza kuiendeleza kwa sababu bado tunaamini kuna maeneo makubwa kwa upande wa Jamhuri yetu hatujafanya utafiti wa kutosha na ambayo yana fursa ya kufanya ugunduzi mkubwa zaidi” alisema Mhe. Balozi Omar  

Kuhusu sekta ya fedha, Mhe. Balozi Omar alisema kuwa Qatar ni Kituo kikubwa cha Fedha (financial Center) katika nchi za Ghuba ya Uajemi, na kwamba Tanzania inaweza kufaidika na uwepo wa kituo kama hicho na kuwezesha kuyafikia masoko ya mitaji.





Share To:

Post A Comment: