Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mha. Wolta Kirita amewataka Mameneja wa Mikoa na Wilaya katika mikoa yote 25 inayohudumiwa na taasisi hiyo kuelekeza nguvu zaidi za kiutendaji katika kuvisimamia na kuvijengea uwezo Vyombo vya Utoaji Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSOs) ili viimarishe utoaji wa huduma hiyo kwa wananchi waishio vijijini na kuchangia uchumi wa nchi.
Mkurugenzi Mkuu Kirita ametoa maelekezo hayo Januari 26, 2026 wakati akizungumza na watumishi wa RUWASA mkoa wa Mara ambako ameanza ziara ya kukagua shughuli za CBWSO na hali ya utoaji huduma ya maji vijijini katika mikoa ya Mara na Mwanza.
Ziara hiyo ni muendelezo wa zoezi la kukagua kazi za vyombo katika kuwahudumia wananchi ambapo Menejimenti ya RUWASA ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu huyo inapita mikoani kutambua na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizopo katika kuwahudumia maji safi ya bomba wananchi wa vijijini.
Akizungumza na watumishi hao wakiongozwa na Meneja wa RUWASA mkoa wa Mara Mha. Charles Pambe na Mameneja wa wilaya za mkoa huo, Mkurugenzi Mkuu Kirita aliwataka kuweka na mpango wa kudumu wa mara kwa mara kuzitembelea CBWSO na kuzisadia pale zinapohitaji msaada wa kiufundi na kitaalamu ili kuzijengea uwezo wa kujua na kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kuondoa changamoto ndogondogo katika kuwahudumia wananchi.
Alisema tangu kuanzishwa kwake mwaka 2019, RUWASA imeshajenga miradi zaidi ya 3,000 ya maji vijijini na kwamba sasa ni wakati muafaka wa kuhakikisha miradi hiyo inakuwa endelevu na unahudumia wananchi maji kwa ufanisi.
Awali, akitoa taarifa ya hali ya huduma ya maji vijijini katika mkoa wa Mara kwa Mkugugenzi Mkuu aliyeambatana na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti, Meneja wa mkoa huo Mha. Pambe alisema wastani wa utoaji wa huduma umefikia asilimia 75 na kwamba ipo miradi inayoendelea kujengwa na itainua zaidi hali ya huduma.
Katika siku ya kwanza ya zoezi la ukaguzi wa CBWSO, Mkurugenzi Mkuu Kirita aliongoza ukaguzi huo katika CBWSO ya Bulisumakwi wilayani Musoma na Kokwe wilayani Rorya.

Post A Comment: