
Na Oscar Assenga, LUSHOTO.
MKUU wa wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Zephania Sumaye ameipongeza Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba wilayani Lushoto kwa kuandaa matembezi y Magamba Walkathon ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuendelea kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo wilayani Lushoto ikiwemo hifadhi hiyo.

Sumaye aliyasema hayo mara baada ya kushiriki mbio hizo ambazo zilikuwa za kilomite 20,10 na 5 huku akieleza matukio kama hayo yanasaidia kuwaweka pamoja na kusaidia kujenga afya na mahusiano kwa jamii mbalimbali zilizopo katika wilaya hiyo na maeneo mengine hapa nchini.

“Tunapoelekea kufunga mwaka matukio kama hayo yanatuleta pamoja na kutusahaulisha na matatizo yao na kujenga afya na kuwaimarisha leo hii nimesimama hapa Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Balozi Batilda Burian ametuma salamu nyingi na kupongeza matembezi haya ambayo yamekuwa na muendelezo kwa kipindi cha miaka mitatu”Alisema

Alisema kwamba anaamini mwakani watafaya kitu kiubwa zaidi ili kuweza kuwavuta watu wengi zaidi kutembelea hifadhi za Lushoto kutokana na uwepo wa vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba.

Awali akizungumza Mwakilishi kutoka Ofisi ya Hifadhi ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Kaskazini kwa niaba ya Kamishna wa (TFS) Kasim Ngemba aliwashukuru wawezeshaji wa tukio hilo wakiwemo wadhamini ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Mkurugenzi,Mhifadhi wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba Lushoto pamoja na wananchi waliojitokeza kufanya tukio hilo kuwa na mafanikio.

Alisema kwamba TFS inasimamia maeneo mengi yanayofaa kwa utalii ikiwemo Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba wilayani Lushoto pamoja na Msitu wa Mkusu ambayo ni mzuri sana na maeneo mengi ya utalii ndani ya Kanda ya kaskazini ikiwemo Tanga wanaweza kupata kiyoyozi cha Mungu kupitia Fukwe ya Bahari wamejenga daraja.

Aidha alisema kwamba kuna misitu mingine katika Kanda hiyo ikiwemo Rau Moshi Mjin,Amani,Chome na Nilo ambapo alitumia wasaa huo kuwahamasisha watanzania watembelee maeneo ya vivutio vya asilia ni vizuri na vinavutia.

“Niishukuru Ofisi ya DC Lushoto kwa ushirikiano ambao wanawaonyesha kuhakikisha suala la Uhifadhi wa maeneo yao Lushoto yanaboreka na kuhakikisha shughuli za uhifadhi zinakwenda vizuri “Alisema

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Mazingira Asili Magamba Christoganus Vyokuta alisema kwamba wametoa fursa kwa wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika maeneo ya Hoteli na Malazi yaliyotengwa kwenye mpango mkakati wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Alisema hivi sasa wana mwekezaji ambaye tayari amekwisha kuwekeza zaidi ya Bilioni 1 huku akiwahamasisha wadau mbalimbali kutembelea hifadhi ya Asili magamba na kuangalia maeneo yenye fursa kiwapatia kipato.

Aidha alisema kwamba utalii ikolojia unakuwa sana nchini kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Serikali kuhamamsisha utalii nchini na hivyo tija kufika mpaka kweye hifadhi hiyo kutokana na idadi ya watalii kuongezeka na kutembea kwao kumechangia kipato cha wananchi wanazunguka hifadhi kuongezeka kwa ujumla.

Alisema kwamba utalii unatija kubwa sana kwa jamii na Taifa kutokana na kwamba katika hifadhi hiyo wageni wengi wanafika kutembelea maeneo ya vivutio mbalimbali kwa kutembea kwao waongozaji watalii wanapata kipato na wananchi kwa ujumla.









Post A Comment: