Wakazi wa Mbezi Beach, Dar es Salaam walishtuka baada ya mwanamke mmoja kugundua kuwa mume wake alikuwa amemwandikisha mwanamke mwingine kwenye bima ya afya ya kampuni alikofanya kazi akimwita “mke wake wa ndoa.” Tukio hilo lilizua taharuki kwa familia hiyo, huku likizua mjadala mkubwa kwenye makundi ya wanawake mtandaoni.

Kwa miaka sita ya ndoa yetu, nilidhani nina mume mwaminifu. Tulikuwa tumepitia mengi pamoja kushiriki ndoto, kupambana na madeni, na hata kupata mtoto mmoja wa kiume.

Sikuwahi hata mara moja kuwa na mashaka juu ya uaminifu wake. Lakini kama wanavyosema, mchana wa ndoa ni mrefu, na ndani yake kuna mawingu yasiyotabirika.

Kisa chote kilianza siku moja nilipoambatana na mume wangu hospitalini baada ya kuumwa ghafla. Alikuwa na bima ya afya ya kazini, hivyo aliwasilisha kadi yake mapokezi. Muda mfupi baadaye, mhasibu wa hospitali alituita pembeni na kuuliza iwapo “mke wa pili” naye angepata huduma. Nilidhani ni makosa ya kawaida ya kiutawala. Soma zaidi hapa 

Share To:

contentproducer

Post A Comment: