Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, ametoa wito kwa nchi za Afrika kuwekeza michango ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii katika miradi ya maendeleo.
Amezungumza hayo katika Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Afrika Leo Julai 10, 2025 uliofunguliwa na Mhe. Dkt. Philip Mipango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika katika kituo cha mikutano AICC jijini Arusha
Mhe. Kikwete amesema mkutano wa nchi wanachama unatoa nafasi ya kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja kwa ajili ya kukuza mifuko hiyo na kuchochea maendeleo ya miundombinu barani Afrika.
Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Mifuko ya Hifadhi ya Jamii: Chachu ya Maendeleo ya Miundombinu na Ukuaji wa Kiuchumi na Kijamii Barani Afrika.”
Post A Comment: