Mwenge wa uhuru umekimbizwa umbali wa Km 222.4  ambapo umetembelea, umekagua, kuweka Jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Sh bilioni 2.2 katika Wilaya ya Longido mkoaniArusha.

Mkuu wa Wilaya ya Longido Salum Hamis Kalli amesema kuwa Mwenge wa Uhuru umefungua vyumba viwili vya madarasa katika Shule msingi Engikaret,mradi wa upandaji miti Mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi Longido (VETA) sambamba na uzinduzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa Km. 0.86'

Pia uzinduzi wa nyumba ya watumishi ( 2 in 1) katika zahanati ya Kimokouwa,kituo cha mafuta Perto Africa, uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa maji Mundarara pamoja na mradi wa uwezeshaji Vijana kiuchumi kikundi cha Umoja Ketumbeine kinachojishughulisha na Uchomeleaji.












Share To:

Post A Comment: