Wakala wa Barabra za mijini na Vijini TARURA wanatarijia zaidi ya bilioni mbili kukamilisha Ujenzi wa Barabara ya TCA Levolisi,CCM, Kaloleni-KwaBenson na TRA Hadi East Africa Zenye Urefu wa Kilomita 2.241 na zitakazojegwa kwa kiwango Cha Lami.
Hayo yamesemwa wakati Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 ulipotembelea na kuweka jiwe la Msingi Katika Mradi huo ambapo Akisoma Taarifa ya Ujenzi huo Mbele ya Kiongozi Wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2025 Ismail Ali Ussi meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Wilaya ya Arusha Mhandisi Godfrey Bwire Amesema Mradi huo unaulianza Tarehe 28.06.2024 huku ikitarajia kukamilika Mwaka huu.
Meneja huyo wa Tarura Amesema Ujenzi huo wa Barabara unalenga kusogeza Huduma ya Miundombinu ya Barabara Kwenye Makazi ya Watu ili kurahisisha Huduma za Usafirishaji kwa kupunguza Gharama za Maisha.
Akizungumza kabla ya kuweka Jiwe la Msingi Katika Barabara hiyo Kiongozi Wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi ameipongeza Tarura kwa kuendelea kumwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza Ahadi za kuboresha Miundombinu pamoja na Utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi wa Barabara kuwa na Ubora unatakiwa.
Aidha Barabara zinazojengwa kwa kiwango Cha Lami ni TCA 0.655km,Levolisi 0.187km,CCM 0.129km,Kaloleni Hadi Kwa Benson 1.0km na TRA Hadi East Afrika 0.27km.
Post A Comment: