Kuna maumivu ambayo hayaonekani kwa macho, lakini huuma rohoni kila siku. Kwa muda wa miaka sita, kila mwezi uliopita bila ujauzito ulijenga ukuta wa huzuni moyoni mwangu.

Niliolewa nikiwa na miaka 27, na kama wanawake wengi, nilikuwa na ndoto ya kuwa mama mara tu baada ya ndoa. Lakini miezi ikawa miaka, na kila matokeo ya “negative” kwenye kipimo cha ujauzito yalikuwa kama kisu moyoni.

Nilifanya kila kitu nilichoambiwa. Nilienda kwa madaktari wa uzazi, nikapima kila vipimo, nikameza dawa hadi nikaanza kuchukia harufu ya vidonge. Mume wangu alinivumilia, lakini niliona majonzi moyoni mwake kila alipokuja kutoka kazini na kunikuta nikilia peke yangu.


Kilichouma zaidi ni maneno ya watu. “Mbona mna miaka mitano bado hamjapata mtoto?” “Huenda huyu dada ana matatizo.” “Amelogwa huyo.” Nilijaribu kupuuza, lakini kila harusi ya rafiki mpya, kila ‘baby shower’ ya jamaa yangu, ilikua kama msumari mpya kwenye kidonda.

Hatimaye, nilikubali hali yangu. Nikawaambia ndugu zangu, “Nimejitolea kulea watoto wa dada yangu, si lazima niwe na wangu.” Lakini ndani ya moyo wangu, kilio hakikukoma. Soma zaidi haapa.


Share To:

contentproducer

Post A Comment: