
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amefanya ukaguzi wa maandalizi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yanayotarajiwa kufanyika tarehe 25 Julai, 2025 katika Uwanja wa Mashujaa, Mtumba Jijini Dodoma.

Mhe. Nderiananga ametembelea Uwanja huo leo tarehe 22 Julai, 2025 ili kujionea maandalizi ambapo amesema yamefikia hatua nzuri inayoridhisha.
Aidha katika maadhimisho hayo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Post A Comment: