Uongozi thabiti na wenye mwelekeo wa pamoja ni nguzo kuu katika utendaji na utekelezaji wenye tija katika katika kufanikisha malengo mapana ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 16 Julai, 2025 katika mafunzo maalum kwa Viongozi wa Wizara hiyo yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha, Mkoani Pwani.

Akifungua mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Sayansi Teknolojia na Elimu ya Juu Prof. Daniel Mushi amesema malengo makuu ya mafunzo ni kukuza uwezo wa kiungozi na utawala, kujenga mshikamano, kujenga misingi ya utendaji katika mwaka mpya wa fedha ulioanza ili kuongeza tija katika kufikia malengo ya kutekeleza mageuzi ya elimu na malengo ya kitaifa ya kuhakikisha kila mtoto anapata Elimu na ujuzi.







Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: