Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 Ndugu Ismail Ali Ussi amewataka walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Ganako Wilayani Karatu kutunza miundombinu ya shule ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa utulivu sanjari na kuhamasisha klabu za kupinga rushwa zinaendelezwa zaidi
Alisema endapo miundombinu ya shule ikitunzwa vema itawezesha wanafunzi kufaulu kutokana na uhalisia wa utulivu uliopo na kusisitiza walimu kusimamia maadili sanjari na kuhamasisha klabu za wapinga rushwa zinaendelezwa ili wanafunzi wajue mbinu mbalimbali za kupambana na rushwa wakiwa mitaani na maeneo mengine.
"Endeleeni kulinda miundombinu ya elimu sanjari na kupinga rushwa kwa wanafunzi lakini naipongeza halmashauri ya wilaya hii kwa kutenga fedha sh, milioni 30 kama mapato ya ndano kwaaajili ya ujenzi wa darasa shule ya msingi Ganako pia endeleeni kujenga na kukarabati madarasa mengine zaidi"
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ganako, Lucy Yamay aliishukuru halmashauri ya wilaya hiyo kutoa sh, milioni 30 kwaaajili ya ujenzi wa chumba kimoja cha darasa kwani mradi huo utawezesha wanafunzi kusoma kwenye mazingira rafiki ikiwemo kupunguza msongamano wa wanafunzi darasa ni
Sambamba na hilo pia alimshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kwakuendelea kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo utatuzi wa changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu , awali Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk, Lameck Ng'ang'a akipokea mwenge huo kutokea wilayani Ngorongoro alisema jumla ya miradi nane ya Bil. 4.6 itazinduliwa, kuwekwa mawe ya msingi sambamba na miradi mingine kutembelewa ikiwemo lishe na matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Post A Comment: