Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega kwenye mjadala wa #MamaNiMjenzi wenye kuangazia mafanikio ya Miaka minne ya serikali ya awamu ya sita kwenye sekta ya Ujenzi, amesema kutekelezwa kwa miradi ya ujenzi nchini, kumenufaisha watanzania wengi zaidi kwa kutoa ajira na manunuzi ya vifaa vya ujenzi kununuliwa nchini.

Waziri Ulega wakati wa mjadala huo uliofanyika katikati ya daraja la Kigongo- Busisi, Miongoni mwa miradi mikubwa iliyotekelezwa na serikali ya awamu ya sita ameeleza kuwa miongoni mwa wanufaika wa miradi hiyo ni kampuni ya Lodhia Group, kiwanda kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani ambacho kimekuwa kikizalisha Nondo ambazo zimekuwa zikitumika kwenye mradi wa ujenzi wa Reli, mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere pamoja na ujenzi wa daraja la Kigongo- Busisi.

Ujenzi wa daraja la Kigongo- Busisi umetekelezwa na kampuni ya China Civil Engineerinh Construction Corporation ikishirikiana na China railway 15 Bureau Group Corporation (CCECC-CR15G JV) ambapo kulingana na Taarifa ya Wizara,zaidi ya asilimia 93 ya ajira zilikuwa za wazawa.

Share To:

Post A Comment: