"Matumizi mengine ikiwa ni ya utalii na watani zangu wasukuma wanaweza kutaka kuja kufanya harusi zao, kurekodi kwaya, kaswida na mambo mengine ya kijamii, kimsingi sisi tumekasimiwa mamlaka na Mhe. Rais kwahiyo mimi ninayo kazi ya kumuomba kwamba yeye na kumjulisha kwamba wapo watanzania wanaotaka kuja kufanya kwaya, kurekodi kuja kufanya mpaka picha za harusi hapa.
Kabla ya kutoa vibali, tutamshirikisha Mhe. Rais na niwahakikishie tukipewa kibali sisi maana yake tutatumia njia ya kuwaambia watanzania wote kuhusu utaratibu maalum kwaajili ya usalama wa watu, watumiaji hao kwasababu hapa malori yatakuwa yanapita tena kwa kasi.
Tumeshaanza kupokea maoni mfano kutoka kwa baadhi ya wabunge wanasema wananchi wasilipishwe lakini malori ya biashara lazima yachangie kwasababu hapa panahitajika hapa maintanance lakini jambo hili halijafika mwisho, linahitaji mjadala na linahitaji kuridhiwa na litakaporidhiwa tutatangaza hadharani."- Mhe. Abdallah Ulega Waziri wa Ujenzi wakati wa mjadala wa #MamaNiMjenzi leo Juni 08, 2025, Jijini Mwanza kwenye daraja la Kigongo-Busisi.
Post A Comment: