Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo wa akizungumza wakati akizundua Jumuiya ya Wanawake wa Nyuklia Tanzania (WiNTZ) jijino Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Atomiki Tanzania (TAEC) Prof.Najat Mohamed akizungumza katika kuhusiana na Uzinduzi wa Jumuiya ya Wanawake Nyuklia Tanzania (WiNTZ) jijinj Dar es Salaam.
Picha za wakati wa uzinduzi WiNTZ katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
IMEELEZWA kuwa licha ya maendeleo makubwa katika sayansi na teknolojia ya nyuklia, ushiriki wa wanawake bado ni mdogo kutokana na changamoto mbalimbali, zikiwemo idadi ndogo ya wasichana wanaochagua masomo ya sayansi, mitazamo ya kijamii, na ukosefu wa mifano ya kuigwa.
Hayo yameelezwa Juni 4, 2025 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, wakati akizindua Jumuiya ya Wanawake katika Nyuklia Tanzania (WiNTz) ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika sekta hii muhimu.
Prof. Nombo amesema kuwa tatizo hilo ni changamoto ya kimataifa, lakini athari zake ni kubwa zaidi katika nchi zinazoendelea.
Ameongeza kuwa WiNTz kimeanzishwa ili kusaidia juhudi za Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) katika kuwawezesha wanawake kwenye sekta ya nyuklia na kuhimiza usawa wa kijinsia katika sayansi na teknolojia. Kwa mujibu wa Prof. Nombo, Jumuiya hii itasimamiwa na Tume ya Nishati ya Atomiki ya Tanzania (TAEC) chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Ameeleza kuwa WiNTz siyo tu Jumuiya, bali ni jukwaa la uwezeshaji, ujumuishi, na ubora ambalo litawezesha wanawake kushiriki maarifa, kusaidiana, na kuleta mabadiliko chanya. Kupitia mpango wa uelekezaji, utetezi, na ushirikiano, chama kitalenga kuwapa wanawake fursa za kitaaluma katika sekta ya nyuklia, ikiwa ni hatua muhimu katika kuinua ushiriki wao na kusukuma mbele maendeleo ya kijamii na kitaaluma.
Katibu Mkuu huyo amesisitiza kuwa hatua hii inaleta matumaini mapya kwa maendeleo ya teknolojia ya nyuklia nchini na nafasi zaidi kwa wanawake katika nyanja hii yenye umuhimu mkubwa.
Aidha Prof.Nombo amesema kuwa serikali imetenga bajeti Bilioni Tatu kwa ajili ya masuala ya Sayansi lengo ni kupata wataalam wengi kutokana na mahitaji yaliyopo hivi sasa.
Hata hivyo serikali imepeleka watanzania sita nje nchu kwa ajili ya kusoma masuala ya Nyuklia wakirudi watafundisha wengine.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Atomiki Tanzania na Rais wa Jumuiya ya Wanawake Katika Nyukilia Tanzania ((WiNTZ) Prof.Najat Mohamed amesema kuanzishwa kwa jumuiya lengo ni kuhamasisha wasichana kusoma masomo ya Sayansi na kuweza kupata wataalam wa Nyuklia.
Amesema kuwa wataalam wa Nyukilia wanahitajika kutokana na kuwepo kazi nyingi hivyo kwa wasichana ni fursa kwao kuingia katika utaalam huo.
Amesema katika majukumu mengine ya Jumuiya hiyo ni kutaka kuwashika vijana wa kike pamoja kuwapa njia ya kufikia ndoto zao katika Nyukilia.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwan Raula Marya amesema kuwa kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo itasaidia katika kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwa watalaam wa Nyuklia.
Amesema katika masuala ya ubunifu ameweza kwenda katika maonesho ya Wanasanyansi nchini Uturuki kwa kuwa na kifaa cha kuvuta Mbu hivyo jitihada zitaongezeka.
Post A Comment: