Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumanne Juni 17, 2025 anatarajiwa kuendelea na ziara yake ya Kikazi Mkoani Simiyu, akipangiwa kufungua kiwanda cha Kuchakata Pamba cha Biosustain Meatu pamoja na miradi mingine ya maendeleo Mkoani humo.
Rais Samia atafungua pia Hospitali ya Wilaya ya Itilima pamoja na kufanya mikutano kadhaa ya hadhara na kuzungumza na wananchi kwenye Kiwanja cha Stendi ya Mabasi Meatu pamoja na Mkutano mwingine utakaofanyika kwenye Kiwanja cha stendi ya Mabasi Itilima mkoani humo.
Jana Rais Samia alizindua kampeni ya Kitaifa ya chanjo na utambuzi wa mifugo, Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Jengo la Halmashauri ya Bariadi Mji, Uzinduzi wa Ofisi za Mamlaka ya mapato Tanzania Mkoa wa Simiyu pamoja na kiwanda cha uzalishaji mabomba na cha uchakataji wa Pamba Mkoani Simiyu. Ziara ya Rais Samia Kanda ya ziwa itampeleka mpaka Jijini Mwanza, alipopangiwa kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo daraja la Kigongo- Busisi Jijini Mwanza.
Post A Comment: