Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu Juni 16, 2025 akiwa Mkoani Simiyu kwenye ziara yake ya kikazi, amezindua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo pamoja na jengo la Halmashauri ya ya Mji wa Bariadi.

Kulingana na Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI, ujenzi na uzinduzi wa majengo hayo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia, ambaye alipoingia madarakanj aliagiza kuboreshwa kwa miundombinu kwenye Mikoa yote 26 ya Tanzania bara ambapo Jumla ya Shilingi Bilioni 91.17 zilitengwa kukarabati na kujenga Ofisi za Mikoa.

Aidha shilingi Bilioni 94.74 zilitengwa kwa Mamlaka za serikali za Mitaa kwaajili ya kujenga na kukarabati majengo ya Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za Miji, Majiji na Wilaya kote Tanzania bara ambapo Mkoa wa Simiyu ulipokea Bilioni 14.10, ambazo zimejenga Majengo manne ya Wakurugenzi, Matano ya wakuu wa Idara pa.oha na jengo la Halmashauri ya Bariadi Mji ambalo limegharimu shilingi Bilioni 3.9

Katika ziara yake Mkoani Simiyu itakayompeleka baadae Mkoani Mwanza, leo pia Rais Samia amepangiwa kufungua shule ya Wasichana Simiyu pamoja na kufungua kampeni ya Kitaifa ya Chanjo na utambuzi wa mifugo na baadae jioni kuhutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara.

Share To:

Post A Comment: