MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa(CCM)Namelock Sokoine amesema tunapokwenda kwenye uchaguzi mjue mnaenda kugombea na si kugombana

Aidha alisema baada ya siasa kuisha kunamaisha mengine hivyo msiumizane katika chaguzi

Namelock aliyasema hayo jana Jijini Arusha wakati wa mapokezi ya kumpokea mjumbe huyo aliyeteuliwa naa Rais Samia Hassan Suluhu kwenye nafasi hiyo ya wajumbe 28 wa Kamati Kuu ukumbi wa CCM Mkoa. 

"Tusiumizane katika chaguzi tupo viongozi hapa ambao tutashiriki katika nafasi za ndani katika michujo tusitumie nafasi zetu kukanyaga wenzetu ambao hawapo katika vikao hivyo, namshukuru Rais Samia kwa kuniteua katika nafasi hii"

Alisisitiza kutoumizana katika uchaguzi huu mkuu wa mwaka 2025 badala yake viongozi wanaoshiriki kuamua katika maamuzi watende haki

Alisema Rais Samia Hassan Suluhu amebeba maono ya haki na usawa hivyo tuwe na hofu ya mungu na tusiumize wenzetu

Alihoji kwanini vijana na watu mbalimbali wanakubali Rais Samia Hassan Suluhu kutukwanwa kwenye mitandao ya kijamii hivyo tusiendekeze matusi na dhihaka kwa Rais wetu tuheshimiane

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, Thomas ole Sabaya alimpongeza Namelock kwa kuteuliwa katika nafasi hiyo ya kuamua maamuzi ngazi za juu na kuongeza kuwa Rais Samia anatoa fedha nyingi mkoani Arusha kwaajili ya miradi ya maendeleo

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda alisisitiza amani katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kuongeza kuwa uchaguzi si kabila wala dini ya mtu bali ni uwezo wa kuchagua mtu mwenye kutatua changamoto


Share To:

Post A Comment: