Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega amesema Wizara yake inatekeleza kikamilifu maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Makandarasi wa ndani wanalipwa fedha zao, akisema kufikia sasa zaidi ya Bilioni 90 zimeshalipwa kwa Makandarasi hao wa ndani wanaotekeleza miradi ya ujenzi.

Waziri Ulega amebainisha hayo leo Jumapili Juni 08, 2025 Jijini Mwanza wakati wa Mjadala wa #MamaNiMjenzi uliofanyika kwenye daraja la Kigongo-Busisi, akibainisha kuwa Rais Samia ameelekeza kuwa kipaumbele cha malipo kwenye Wizara hiyo kuwa kwa Makandarasi wazawa wanaoidai serikali.

 "Ukweli ni kwamba kazi ya kuwalipa inaendelea hatua kwa hatua na kwenye jambo hili ukweli ni kwamba tunaendelea kuongeza kasi na nimewaeleza wataalamu wangu pale Wizarani kwamba hata fedha ikija kidogo kipaumbele cha kwanza kiwe ni kuwalipa wakandarasi wa ndani kwasababu uchumi unazunguka humu ndani, tutawalipa na yote yatakwisha." Amebainisha Waziri Ulega.

Share To:

Post A Comment: