Na.Ashura Mohamed - Arusha 

Katika kuhakikisha kuwa Uchumi wa wakazi wa mkoa wa Arusha  unaimarika  wananchi wa mkoa huo hususani Vijana  wametakiwa kuhakikisha kuwa wanachangamkia fursa mbali mbali za kiuchumi ili kunufaika na ujio wa mashindano ya kimataifa ya Afcon 2027.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini bw.Jospeh Mkude,wakati wa Kongamano la Vijana  la Engutoto Youth Summit kuhusu Mashindano ya AFCON 2027,Wakili Irene Ndosi ambaye ni Katibu Tarafa Suye  amesema kuwa ujio wa Afcon ni neema kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Arusha ambapo mbali na kupata burudani ya mpira wa miguu lakini pia ni fursa kwa makundi yote kuongeza uchumi wao.

"Fursa zitaanzia kuanzia watu wa chini kabisa boda boda,watu wa usafirishaji mpaka wanawake watengeneza shanga,kila mtu achukue nafasi hiyo kuleta mabadiliko chanya  kwenye uchumi wake binafsi na familia yake na mkoa  kwa ujumla,pia tuwe tayari kujaza eneo la  uwanja wa Afcon kwasababu mashindano haya ni yakipekee na yanashirika nchi tatu ambazo ni Tanzania,Kenya na Uganda."Amesitiza Ndosi 

Aidha Hamza Juma Njiku ni Diwani wa Kata ya Engutoto amesema kuwa kongamano hilo ni muhimu kwa kuwa limewakutananisha vijana na wadau mbal8 mbali katika kuonyesha fursa zilizopo kuelekea mashindano hayo ya Afcon.

"Sisi katika kata yetu fursa za Afcon zimetugusa moja kwa moja kwa kuwa tunajengewa Uwanja mkubwa mzuri wa Mazoezi kwaajili ya mashindano hayo ambapo utakuwa na uwezo wa kuchukuwa watu 5000 waliokaa,maegesho ya magari 500 na mabasi mawili kwaajili ya zile timu ambazo zitaingia kufanya mazoezi,ila uwanja ukikamilika na mashindano kumalizika utatumika kwaajili ya ligi kuu na michuano mbali mbali."Amesema Diwani Njiku

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM),Kata ya Engutoto ambaye ndio muandaaji wa Kongamano Engutoto Youth Summit,bw.Ibzan  Michael Ruheta  amesema kuwa  kongamano hili si jukwaa la kisiasa bali ni jukwaa linalokutanisha watu wote kujadili fursa za AFCON kuelekea mwaka 2027. 

Bw.Ruheta  amesema kuwa Mashindano ya AFCON hayatahuishwa na Tanzania peke yake bali ushirikiano na  mataifa mengine wakiwemo Kenya pamoja na Uganda,hivyo kama Watanzania ni wajibu wao  kuamka na kuhakikisha tunaitumia nafasi hiyo ipasavyo.

"Ndugu mgeni rasmi, kama unavyojua nchi yetu imepata fursa ya kuandaa mashindano haya ya AFCON,hivyo kama viongozi mliopo katika nafasi za maamuzi, ni vizuri kujipanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na taasisi mbalimbali zilizopo nchi yetu kwa kikisha fursa hizi tunazipata kwa wakati, vijana waheshimiwe, wasikilizwe na kero zao zitatuliwe ili nchi yetu inufaike."Amefafanua  Mwenyekiti huyo

Kongamano la Engutoto Youth  Summit lenye kauli mbiu ya "Unlocking 2027 AFCON Opportunity" limeandaliwa na Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Engutoto,na limekusudia kuwajengea vijana uwezo wa kunufaika na fursa za michezo hiyo kubwa ya kimataifa ambapo limefanyika katika Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) na kukutanisha Vijana Zaidi ya 1000 ili kuonesha nyanja mbali mbali ambazo vijana wanaweza kunuifa nazo.








Share To:

Post A Comment: