MFUKO wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) umewataka waajiri kuhakikisha wanalipa michango yao kwa wakati kwa watumishi wao na wasisubiri mpaka wapelekwe mahakamani kutokana na kutokuiwasilisha .
Hayo yalisemwa leo na Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga Nuhu Mbaga katika maonyesho ya 11 ya Biashara na Utalii yanayoendelea katika eneo la Mwahako Jijini Tanga.
Ambapo alisema wanashiriki maonyesho hayo kwa lengo la kutoe elimu kwa wananchi juu ya mafao mbalimbali wanayoyatoa wanapojiunga nao. imewataka waajiri mkoani Tanga kuhakikisha wanalipa michango ya wafanyakazi wao ili waweze kupata sifa za kupata mafao yao pindi wanapostaafu.
Alisema kwamba wanatakiwa kulipa michango kwa sababu ipo kwa mujibu wa sheria na wasipofanya hivyo kifungu cha 72 wanaweza kukitumia kwa ajili ya wao kupelekwa mahakamani.
“Hivyo nitumie nafasi hii kuwataka waajiri tusisubiri mpaka mpelekwe mahakamani bali wahakikisheni mnatekeleza wajibu wenu kupeleka michango ya watumishi wenu”Alisema
Aidha alitumia wasaa huo kuwahamasisha wananchi waliojiajiri kufika kwenye banda lao kuweza kupata elimu ya kuweza kujiunga na kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa kwenye mfuko huo ikiwemo ya kupata matibabu kama ilivyo kwa wengine
“Yote haya ni kutokana na sera nzuri ya awamu ya sita chiini ya Rais Dkt Samia Suluhu kwa sababu mtu akiwa na afya njema ataweza kwenda kujishughulisha na kufanya kazi ya kupata kipato cha mtu mmoja mmja na kuweza kujikwamua kiuchumi”Alisema
Post A Comment: