Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Laban Kihongosi ameahidi kuendelea kutekeleza maelekezo na maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan, akimshukuru kwa kuridhi na kutoa zaidi ya Shilingi Bilioni 60, kutekeleza miradi na huduma mbalimbali za Maendeleo kwenye Wilaya ya Meatu Mkoani humo.
Mhe. Kenani amebainisha hayo leo Jumanne Juni 17, 2025 wakati akitoa salamu za Mkoa kwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake Wilayani Meatu Mkoani Simiyu akieleza kuwa fedha hizo zimetekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Daraja la Itembe lililogharimu Bilioni 8.4 pamoja na ruzuku ambazo zimekuwa zikitolewa kwenye mbolea, mbegu na viuatilifu kwenye zao la Pamba
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Meatu Mhe. Leah Komanya amemshukuru Rais Samia kwa utekelezaji mkubwa wa maboresho katika huduma za afya Meatu pamoja na utekelezaji wa mradi mkubwa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (Simiyu Climate Resilience Project) katika wilaya tano za Mkoa wa Simiyu, akisema mradi huo utaondoa changamoto kubwa ya uhitaji wa maji iliyotokana na ukame Wilayani Meatu.
Aidha Mbunge wa Kisesa Mhe. Luaga Mpina, amempongeza Rais Samia kwa kwa maboresho makubwa kwenye mifumo ya kodi nchini, akimuomba Rais Samia kuharakisha ujenzi wa Treni ya kisasa ya SGR ili kuongeza thamani na faida kwa wakulima na wafugaji wa Kanda ya Ziwa ikiwemo Mkoani Simiyu.Luaga ameeleza kuwa wananchi wa Kisesa na Meatu kwaujumla wameahidi kumpa kura za kishindo Rais Samia katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Post A Comment: