"Ndugu zangu nimejulishwa kuwa jumla ya wataalamu wa mifugo takribani 3800 watashiriki moja kwa moja kwenye kampeni hii katika maeneo mbalimbali nchini. Kutokana na uhaba wa maafisa wa ugani wa mifugo katika Mamlaka za serikali za mitaa, mpango uliopo unaenda kutoa pia fursa za ajira za muda mfupi 7500 kwa vijana wetu, wataalamu wa mifugo hususani Vijana waliopo nje ya mfumo wa ajira au ajira rasmi.
Sasa ninawasihi watambue kwamba wamekabidhiwa jukumu kubwa hilo wakahudumie mifugo yetu hiyo kwa weledi na kwa uzalendo ili kupata matokeo yanayotarajiwa. Tukifanya vinginevyo tutakuja kulaumu wazalishaji wa chanjo kumbe uchanjwaji umekosewa, kwahiyo niwaombe sana wale wote watakaoshiriki kwenye zoezi hili wafanye kadri watakavyoelekezwa na wataalamu.
Hatutarajii kujitokeza kwa uzembe katika kuhudumia maisha ya mifugo yetu aidha kwa mara nyingine tena niwatake wafugaji kujitokeza kwa wingi kupeleka mifugo katika maeneo ya chanjo na utambuzi."- Rais Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza na wananchi wa Bariadi Mkoani Simiyu, mara baada ya kuzindua Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo na utambuzi wa mifugo leo Juni 16, 2025.
Post A Comment: