Na. Peter Haule, Singida.
Wizara ya Fedha imeng'ara kwenye Sherehe ya Wafanyakazi (Mei Mosi) Kitaifa, baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa mchezo wa mpira wa miguu katika mashindano yaliyoshirikisha Wizara na Taasisi za Serikali.
Tuzo za washindi katika mashindano mbalimbali zimetolewa na Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe za Mei Mosi Kitaifa, zilizofanyika katika Viwanja vya Bombadia Mkoani Singida.
Akizungumza wakati wa maandamano ya wafanyakazi wa Wizara ya Fedha walioshiriki katika sherehe hizo, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Wizara ya Fedha, Bw. Shumbi Mkumbo, alisema kuwa Wizara ya Fedha imenyakua tuzo mbili ikiwemo hiyo ya mshindi wa mpira wa miguu na tuzo ya uendeshaji Baskeli, jambo lililo chochea hamasa kwa watumishi wa Wizara kushiriki zaidi katika michezo.
Alisema kuwa Wizara itaendelea kuhamasisha michezo kwa kuwa inaimarisha afya kwa watumishi na pia inahimiza umoja na mshikamano.
Sherehe hizo kwa Wizara ya Fedha zimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Naibu Katibu Mkuu, Bi. Jenifa Christian Omolo na Mkurungenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali watu, Bi. Fauzia Nombo.
Post A Comment: