Wanawake kikundi cha UMOJA kilichopo Wilaya ya Mtama Mkoani Lindi wamejengewa uwezo na Mtaalam kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) juu ya ufugaji bora wa nyuki na uongezaji thamani mazao ya nyuki ambapo wameweza kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile Sabuni, Mafuta ya kujipaka , mishumaa ambazo zinatokana mazao ya nyuki (asali na nta)
Bi Amina Nandilika ambaye ni Mwenyekiti wa kikundi hicho amesema mafunzo hayo Yana tija katika kuongeza kipato chao kwani awali walikua wakinufaika na asali pekee “ mafunzo haya yatatuwezesha kuandaa bidhaa nyingi zaidi kwa ubora wa juu” amefafanua Nandilika
Mtafiti kutoka TAWIRI Bw. Jackson Vicent Kizeze amesema tafiti za nyuki zinazofanywa na TAWIRI kupitia Kituo cha utafiti wa wanyamapori Njiro zinalenga kupata taarifa za kisayansi zinazosaidia kuleta tija katika Sekta ya nyuki ambapo amewakaribisha wadau na jamii kuja TAWIRI ili kujifunza juu ya ufugaji bora wa nyuki na uongezaji thamani mazao ya nyuki.
Post A Comment: