Na Oscar Assenga,TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian amesema
kwamba takwimu ni nguzo na nyenzo muhimu katika kupanda utekelezaji wa mipango
mbalimbali maendeleo duniani.
Dkt Batilda aliyasema hayo leo Jijini Tanga wakati
akifungua mkutano wa kwanza wa Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu nchini (NBS) ambapo alisema kwamba mabazara hayo yana maada mkubwa
kwa wafanyakazi.
Ambapo alisema kwamba Serikali inatambua jukumu hilo
kubwa la (NBS) kuzalisha na kusambaza pamoja na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu
wa takwimu rasmi kwa ajili ya kupanda utekelezaji wa mipango mbalimbali ya
maendeleo katika nchi.
Alisema kutokana na hilo wanamshukuru Rais Dkt Samia
Suluhu kwa utashi wake mkubwa wa kisiasa alionao katika kuendeleza Tasnia ya Takwimu
nchini na wote wameona mafanikio yake .
“Wote tunaona kwa namna ya kipekee Serikali ya awamu ya sita imekuwa mstari wa mbele kuwezesha uzalishaji
wa takwimu rasmi pamoja na matumizi ya takwimu katika mipango mbalimbali ya
maendeleo na Dira bila takwimu hakuna kinachoendelea”Alisema
Hata hivyo aliipongeza timu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa umoja na mshikamano kutokana na takwimu huanzia
katika uzalishaji,uchakataji wake,uhakiki wake mpaka usambazaji wake kutokana
na kwamba mtu moja hawezi kufanya pekee
yake hivyo lazima wafanye kazi kwa ushirikiano.
Alisema kwamba wanaendelea kuhamasisha wenzao wajiunge
kwebye vyama vya wafan yakazi hasa tughe ili waweze na kauli kubwa ambavyo
itakuwa na maslahi mapana kwa nchi na sisi wenyewe.
Aidha aliwataka kuhakikisha wanafanya kazi kwa tija na
uzalendo na kuongea nao waelewe dira na dhima ya taasisi zao na mambo ambayo
hawataji kuyaona kwenye taasisi zao ikiwemo uvujaji wa siri.
“Katika mambo ambayo tunawapongeza sana NBS ni usiri
mkubwa mlionao kwa kweli mnafanya kazi kubwa na sasa wanakwenda kwenye
teknolojia ya habari tunaweza kuwa na usiri lakini mkaingiliwa kuna viti ya
kimtandao inabidi tuendelee kujiimarisha sana kwa maana nyie ndio wamebeba roho
ya nchi”Alisema
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwa sababu taarifa zote zipo
kwao kwa hiyo wajipange na moja ya maeneo ambayo watapaleka watu wengi kusoma
ni masuala ya ulinzi wa kimtandao ili kuungana na kikosi kazi cha Serikali ili kuhakikisha kwamba taarifa zinakuwa
salama na hakuna jambo ambalo litaingizwa.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi
(NBS) na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt Amina Msengwa alimshukru Rais Dkt Samia
Suluhu kwa kumteua kuwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali anatambua heshima kubwa
aliyopewa na kuhaidi kuendelea kusimamia ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa
maelekezo na waledi mkubwa ili kuhakikisha majukumu ya NBS yanakwenda sambamba
na kasi ya maendeleo ya Rais.
“Nimshukuru Kamisaa Anna Makinda kwa kuendelea
kutusaidia katika ushauri lakini kusimamia mkakati wetu wa usambazaji wa
matokeo ya Sensa na tunaendelea kujivunia kutoka kwake”Alisema
Aidha alisema kwamba kupitia ofisi ya Taifa ya Takwimu
wanataka kuijenga Tanzania yenye maendeleo ya juu kabisa huku akieleza kwamba
wamekuwa wakitekeleza sheria na kanuni za zinazoongoza uundaaji na
uendeshaji na u vikao vya mabaraza la
wafanyakazi .
Naye kwa upande wake Kamisa wa Sensa na Spika wa Bunge
Mstaafu Anna Makinda alisema baraza la
wafanyakazi ndio roho muhimu ambayo inaunganisha wafanyakazi na menejimenti ambapo
alitumia wasaa huo kuwataka watumishi kujiunga kwenye mabaraza hayo kutokana na
uwepo wa manufaa mbalimbali.
Mwisho
Post A Comment: