Tanzania na Finland zimekubaliana kuendelea kushirikiana na kuimarisha ushirikiano wao kwenye Elimu ya kidigitali pamoja na ukuzaji wa vituo atamizi (Incubation Hubs) kwaajili ya kampuni changa zilizopo nchini Tanzania.
Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mazungumzo ya Marais wa nchi hizo mbili, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Rais Alexander Stubb, wakati wa mazungumzo yao mara baada ya Rais Stubb kuwasili nchini Tanzania leo Jumatano Mei 14, 2025 kwaajili ya ziara ya kikazi kufuatia mualiko wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Vilevile ni dhamira yetu kuona namna tunavyoweza kushirikiana kukuza zaidi matumizi ya TEHAMA kwenye sekta muhimu za uzalishaji kuendana na mikakati yetu ya Kidigitali." Amesema Rais Samia.
Mbele ya wanahabari mara baada ya mazungumzo yao Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa majadiliano yao yameimarisha pia mahusiano katika sekta muhimu ikiwa pia ni pamoja na kusaidia katika uimarishaji wa huduma za serikali mtandao na usalama wa mtandao.
Katika mazungumzo yao, Rais Samia pia amemuahidi Rais Stubb kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Finland kwenye Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya Kimataifa katika kuhakikisha kuwa wanalinda amani na ustawi wa watu wa Mataifa hayo mawili yenye urafiki wa zaidi ya miaka sitini kwa hivi sasa.
Awali Rais Stubb amemueleza Rais Samia kuwa Finland kwasasa inafanya kazi na Mataifa mawili pekee barani Afrika ambayo ni Tanzania pamoja na Ethiopia, suala ambalo linadhihirisha mahusiano ya dhati miongoni mwa mataifa hayo mawili yaliyo rafiki.
Post A Comment: