Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Amir Mohammed Mkalipa amewataka watumishi wa umma Wilayani Arumeru kufanyakazi kwa moyo wa kizalendo nyakati zote za utumishi wao ili kuwa kielelezo kwa vizazi vijavyo.

Mkalipa amesema hayo wakati wa sherehe mahafali ya 8 ya kidato cha sita ikiwa sambamba na  sherehe ya kumuaga rasmi Mkuu wa Shule hiyo Ndg.John Massawe aliyehudumu shuleni hapo Kwa Miaka 21.

Akizungumzia suala la uzalendo,,mhe.Mkalipa amesema kuwa Mwl.Masawe amekuwa kielelezo cha utumishi uliotukuka kwani shule hiyo imekuwa mara kwa mara ikifanya vizuri katika ufaulu wa Kitaifa chini ya usimamizi wa Mkuu huyo wa Shule mstaafu kwani wanafunzi wamekuwa wakipata ufaulu wa madaraja ya juu, huku akimtaka Mkuu wa shule mpya pamoja na wanafunzi kuendeleza juhudi ili kulinda hadhi ya shule hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Bi Nai Molle ameongeza kwa kusema kuwa mkuu huyo wa shule Mwl.John Massawe ni mfano wa kuigwa na Kiongozi wa kipekee ambae amemudu kufanya kazu katika mazingira magumu na ambayo ameweza kuyabadilisha na sasa ni kivutio na shule ya mfano Kitaifa.

Ameongeza kusema kuwa walimu wa shule ya sekondari Mwandet, wanajuhudi kubwa katika kuwafundisha watoto, na matokeo ya juhudi hizo yanaonekana wazi jambo ambalo limetugusa wazazi wote, na kufanya maamuzi ya kumnunulia gari Mkuu wa Shule John Massawe ikiwa ni shukrani kwa kazi nzuri aliyofanya Kwa Miaka 21 ya Utumishi wake.

"Shule ya Mwandeti ni kubwa, ina walimu wengi, haina nyumba za kutosha kuishi walimu wote hapo shuleni, lakini pia eneo hili halina nyumba za kupangisha, hivyo asilimia kubwa ya walimu hulazimika kuishi Ngaramtoni, huku kukiwa hakuna usafiri wa kuaminika kufika shuleni, walimu wanateseka sana, wazazi tumeamua kuwaondolea adha hiyo wakati wakiwahudumia watoto wetu" amesisitiza Mwenyekiti huyo.

Aidha amefafanua kuwa Mkuu wa Shule John Massawe alihamasiaha ununuzi wa gari aina ya coaster ambao, umegharimu kiasi cha shilingi milioni 48, fedha zilizopatikana kwa kila wazazi kuchanga kiasi cha shilingi elfu thelathini, jambo ambalo limefanyika kwa muda wa miezi miwili baada ya makubaliano ya kikao cha wazazi wote.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha, bwana Seleman Msumi, amempongeza mwl.John Massawe  na kusema moja ya kitu alichofanya ni kuunganisha wazazi na walimu kuwa kitu kimoja na hususan katika kuinua taaluma shuleni hapo pamoja kuifanya shule kuwa moja ya shule bora Nchini kwa matokeo ya mitihani ya kidato cha 4 na 6. 

Mkurugenzi Msumi, amefafanua kuwa, kutokana na Jiografia ya Halmashauri ya Arusha, walimu wa shule nyingi za pembezoni wanakabiliwa na changamoto ya nyumba za kuishi pamoja na usafiri wa kufika shuleni, licha ya kuwa walimu hao, hujitoa kwa hali na mali, kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa kufundisha wanafunzi kwa kuweka uzalendo mbele.

Aidha amewasihi wazazi wengine kuigana mfano huo uliofanywa na wazazi wa Mwandet sambamba na kuwataka wadau wa elimu, kujitokeza kuisaidi serikali kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu, hususani katika ujenzi wa nyumba za walimu pamoja na usafiri.

Hata hivyo mkuu huyo wa shule sekondari Mwandet, mwalimu John Masawe amewashukuru wazazi ,waalimu,watumishi na wanafunzi kwa kutambua na kuthamini kazi kubwa aliyofanya kama Mkuu wa shule kwa kushirikiana na wallimu walio chini yake na kuwaomba  kuendelea  kuchapa kazi ili kupataa matokeo maazuri kwa wanafunzi ili waweze kutimiza ndoto zao.

Shule ya sekondari Mwandet ni miongoni mwa shule za Kata, inayoendelea kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kitaifa, huku ikiwa ni miongozi wa shule 10 bora kitaifa kwa miaka mitatu mfululizo kwa matokeo ya kidato cha sita

Share To:

Post A Comment: