
MENEJA wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Mafuta (EWURA) Kanda ya Ziwa Bw.George Mhina,akizungumza wakati wa semina ya wadau wa biashara ya mafuta iliyofanyika ukumbi wa ELCT-Bukoba, mkoani Kagera leo 13 Machi 2025.
Na.Mwandishi Wetu-Bukoba
MENEJA wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Mafuta (EWURA) Kanda ya Ziwa Bw.George Mhina amewakumbusha wadau kufuata sheria, kanuni, na taratibu katika kuendesha biashara ya mafuta hapa nchini wakati wa semina ya wadau iliyofanyika ukumbi wa ELCT-Bukoba, mkoani Kagera leo 13 Machi 2025.
Semina hiyo iliyolenga kutoa elimu kuhusu utaratibu wa kuomba leseni na udhibiti wa biashara ya mafuta na gesi ya kupikia, imejumuisha washiriki kutoka sekta binafsi na serikali mkoani Kagera.
"Wadau wa biashara ya Mafuta wanatakiwa kufuata kanuni,taratibu na Sheria ambayo imekuwa ikitolewa na EWURA ili wasikutane na mkono wa sheria."amesema Mhina
Washiriki wameishukuru EWURA kwa mafunzo hayo ambayo yamewapa fursa ya kuwasilisha kero na ushauri kwa Mamlaka huku wakiomba mafunzo ya aina hiyo kuwa endelevu.















Post A Comment: