Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala na Fedha ya Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), CPA Constantine Mashoko ameitaka Menejimenti ya taasisi hiyo kukamilisha mchakato wa upatikanaji wa Ithibati wa Vyungu vinavyo tutumika kuyeyushia sampuli za madini ya dhahabu.

CPA Mashoko ameyasema hayo leo Oktoba 22, 2024 kwenye kikao cha Kamati wakati akipokea Ripoti ya Utawala na Fedha kilichofanyika katika ukumbi wa Prof. Abdulkarim Mruma uliyopo Jijini Dodoma.

Aidha, CPA Mashoko amebariki pendekezo la Menejimenti la kuiomba Serikali kutumia Sheria ya Local Content ili kuwataka wadau kutumia Vyungu vya kuyeyushia sampuli za Dhahabu kutoka ndani ya Nchi kwa asilimia kadhaa ya mahitaji yao.

Aidha, imeelezwa kuwa,  kutokana na umuhimu wa usalama wa sampuli katika kutoa majibu sahihi, wadau wengi walioko sokoni, wanahitaji Vyungu imara na vyenye ubora uliodhibitishwa na Taasisi za udhibiti Ubora zinazoaminika Kimataifa ambapo, vyungu vinavyotengenezwa na GST vina ubora wa hali ya juu na vipo katika hatua za mwisho za kupata Ithibati hiyo.

Pamoja na mambo mengine, Taarifa mbalimbali za utekelezaji kwa kipindi kinachoanzia Julai hadi Septemba, 2025 zimewasilishwa katika Kamati hiyo ambapo Meneja wa Fedha kutoka GST amewasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Sehemu ya Fedha na Uhasibu, Meneja wa Utawala na Rasilimaliwatu Jacqueline Kalua amewasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Sehemu ya Usimamizi na Maendeleo ya Rasilimalwatu na Utawala;

Pia, Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Datus Matuma amewasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi na Meneja wa Mipango na Masoko Priscus Benard amewasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Sehemu ya Mipango na Masoko.

Vikao vya Kamati vya GST ni maandalizi ya vikao vya Bodi vinavyofanyika mara nne kwa Mwaka ambapo ni kila baada ya kila Robo ya Mwaka wa Fedha ambapo kwa taasisi ya GST kuna jumla ya Kamati tatu ikiwemo Kamati ya Jiosayansi, Kamati ya Ukaguzi na Kamati ya Fedha na Utawala.


Share To:

Post A Comment: