Na Okuly Julius Dodoma
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ( (NEEC) Being'i Issa amesema maonesho ya Mfuko na Program za uwezeshaji wananchi kiuchumi mwaka huu yatafanyika mkoani Singida kuanzia Septemba 8 hadi 14 mwaka huu.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari leo Agosti 27,2024 amesema kuwa maonesho hayo yatafunguliwa mkoani Singida Septemba 8 na afungwa Septemba 14 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kuwa mkoa wa Singida na mikoa jirani ya Dodoma, Tabora na Shinyanga itashiriki.
Amesema kuwa maonesho hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka na mwaka Jana yalifanyika mkoani Kigoma.
Amesema kuwa kuna jumla ya mifuko ya uwezeshaji 64 na programu za uwezeshaji nane na zote zinatarajiwa kushirki maonesho hayo.
"Tunawakaribisha wananchi wa Singida na mikoa jirani, hiyo ni fursa ya wananchi kujifunza na amna ya kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika Mkoa kwa ajili ya kujiinua, kujiendeleza,kujiimarisha kiuchumi pia kujifunza mikopo inayotolewa na Baraza ambazo riba zake ziko chini,"amesema.
Amesema kuwa madhumuni ya maonesho hayo ni kupeleka huduma karibu na wananchi.
"Tunatarajia zaidi ya wananchi 10,000 watajitokeza katika kutembelea maonesho hayo na kujifunza.,"amesema.
Pia amesema wakati wa maonesho kutakuwa na darasa la mafunzo yatakayotolewa bure na Benki kuu ya Tanzania (BOT)
"BOT ni mdau mkubwa sana na wamekuwa wakihakikisha elimu ya fedha inakwenda kwa jamii ,"amesema
Post A Comment: