Serikali imepeleka zaidi ya shilingi Bilioni moja katika Kata mbili za Noondoto na Kimokouwa zilizopo Wilayani Longido Mkoani Arusha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa nane,maabara tatu za Sayansi,jengo la utawala na ujenzi wa vyoo vya walimu na wanafunzi kwa Kata hizo.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Longido ,Dkt Steven Kiruswa katika Mkutano wa hadhara katika kata ya Noondoto katika ziara zake za kusikiliza kero za wananchi na kusema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameitendea haki Longido na wananchi wa jimbo hilo wamemshukuru sana kwa kiasi hicho cha fedha.

Alisema Kata ya Noondoto ambayo iko umbali wa zaidi ya km 90 kutoka Longido mjini imepewa shilingi milioni 584 na kata ya Kimokouwa nayo imepewa kiasi hicho hicho  kwa hali hiyo unaona kabisa ni jinsi gani serikali ya Rais Samia inavyowajali wananchi wa Longido na nchi kwa ujumla katika suala la elimu na wananchi wanapaswa kupeleka Watoto shule ikiwa ni njia mojawapo ya kumuunga mkono.

Waziri huyo alisema katika kuunga mkono jitihada za Rais katika suala la elimu,wananchi wa kata ya Noondoto wametumia nguvu kazi kwa kuzomba kokoto,mchanga,mawe zenye thamani ya shilingi milioni 6.8 na zaidi ya shilingi milioni 70   zimechangwa kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya shule hiyo ikiwemo bweni la wasichana na wavulana.

Alisema wananchi wa kata hiyo wanastahili kupongezwa katika jitihada hizo na kukaa na kusubiri msaada kutoka serikalini hiyo sio sawa na uamuzi wa kutumia nguvu kazi kwa kuleta Kokoto,mchanga,mawe vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni8 wanastahili kupongezwa na kata nyingine zinapaswa kuiga mfano wa Noondoto.

‘’Kwa niaba ya wananchi wa Longido tunakushuru sana Rais kwa msaada wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule na hivyo wananchi hawatakuangusha katika uchaguzi ujao na niwapongeza wananchi kwa nguvu kazi ya ujenzi wa mabweni mawili kwani mnastahili pongezi za dhati ’’

Naye Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Longido,Gilbert Sombe alisema kuwa Longido imepata bahati sana kwani ndani ya muda mfupi sekondari tano zimejengwa na Serikali za kidatu cha kwanza hadi cha nne lengo ni kutaka wilaya hiyo kuwa na shule za sekondari 15.

Sombe alisema wilaya ya Longido ilikuwa ya sekondari moja ya kidatu cha sita lakini sasa Serikali imedhamiria kujenga shule za kidatu hicho shule tatu na yote hayo yanafanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia hivyo wananchi wa Longido mnapaswa kumpongeza na kumshukuru kwa kuwapendelea katika suala la elimu.

Alisema wilaya ya Longido inahitaji sana shule za bweni kutokana na Miundombinu yake na jamii ya kifugaji inapaswa kushirikiana na serikali katika kuwapeleka watoto shule kwani serika inawajali na kuwathamini.

Naye Afisa Mazingira wilaya ya Longido ,Elimeriki Ukwan ujenzi wa shule na mabweni mawili ndani ya eneo la ekari 39 umezingatia kila kitu katika kuhifadhi Mazingira  .










Share To:

Post A Comment: