Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  Nape Moses  Nnauye amewataka wakazi wa wilaya ya Geita Mkoani humo kuhakikisha wanatumia Teknolojia ya Mawasiliano kama fursa na si kutumia Teknolojia  kuvunja ndoa kwani Teknolojia huacha alama.


Ameyazungumza hayo Mara baada ya kukagua na kuzindua Minara miwili ya Mawasiliano ukiwemo Mnara ulioko wilayani Geita na Mnara uliopo wilayani Bukombe ambapo amesema Serikali imeleta kiasi cha Fedha shilingi Bilioni 2.2 kwa ajili ya kutatua changamoto ya Mawasiliano ndani ya mkoa wa Geita.

" Kama alivyosema Mkuu wa Mkoa kwa Mkoa wa Geita Rais Samia ameleta shilingi Bilioni 2.2 kwa ajili ya kuhakikisha wananchi mkiwemo nyie mnaweza kuwasiliana kutokea hapa kijijini mtu asikudanganye teknolojia inaacha alama msije mkaitumia kuleta Matatizo yako maeneo mengine tumewapelekea minara tumewapelekea teknolojia imegeuka kuwa tabu kwa kwenye ndoa zao , " Waziri Nnauye.

Nnauye amesema matarajio ya Serikali ni kujenga jumla ya minara 758 kupitia Mfuko wa mradi wa Miundombinu ambayo inajengwa Tanzania bara katika mikoa 26 huku akisema Serikali inatoa ruzuku zaidi ya Bilioni 266 ya ujenzi wa Minara hiyo.
Share To:

JOEL MADUKA

Post A Comment: