Serikali kupitia mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imetoa ruzuku ya Sh2.2 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa minara 17 mkoani Geita kwenye mradi wa ujenzi wa minara 758 katika mikoa 26 ya Tanzania Bara.
Ujenzi wa minara hiyo 17 itanufaisha kata 16, vijiji 27 huku wananchi 241,240 wanaoishi vijijini watanufaika na huduma ya mawasiliano mkoani humo.
Hayo yamesemwa leo Julai 17, 2024 mjini Geita wakati Waziri wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alipokuwa akipewa taarifa ya hali ya mawasiliano ya mkoa huo alipotembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Juni, 2024 tayari jumla ya minara 6 imewashwa mkoani humo na inatoa huduma ya mawasiliano kwa teknolojia ya 2G, 3G na 4G.
Vijiji ambavyo vimeanza kunufaika ni katika Kaya ya Busonzo, Iyogelo, Makurugusi, Nyakagomba, Ilolangulu na Nhomolwa
Nape anaendelea na ziara yake ya kukaguwa kazi ya ujenzi wa minara 758 inayojengwa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo zaidi ya wanakijiji 8.5 milioni nchini watanufaika na mradi huo.
Post A Comment: