Na Denis Chambi, Tanga.
KUELEKEA uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa wa mwaka 2024 na ule wa madiwani, wabunge na Rais utakaofanyika mwaka 2025 mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Husna Sekiboko amewataka umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi 'CCM' kutumia vyema falsafa nne '4R' za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuanzia mchakato wa uchaguzi ndani ya Chama hicho
Falsafa hizo ambazo ni Reconciliation (Maridhiano) ,Resilience (Ustahimilivu) , Reform (Mabadiliko) na Rebuild (Kujenga upya) amesema zikitekelezwa vyema zitawezeaha kuzidi kukiimarisha chama hicho kuelekea chaguzi zote zitakazofanyika..
Sekiboko ametoa wito wakati wa mkutano wa Baraza wa wajumbe wa mkutano mkuu wa umoja wa wanawake 'UWT' mkoa wa Tanga ulioongozwa na Mwenyekiti wake Alshaymaa Kwegyir ambapo ametoa simu janja 10 kwa Kila jumuiya zenye thamani ya shilingi Milion12 katika wilaya zote 9 za mkoa huo zitakazotumika kwaajili ya kusajili wanachama wapya kwa njia ya kielektroniki ili kuongeza idadi yao na kuwawezesha kushinda kwenye chaguzi zote kuanzia ngazi ya vijiji, vitongoji na mitaa.
"Mwenyekiti wetu wa chama Cha Mapinduzi Taifa Dkt Samia Suluhi Hassan ameweka mkazo sana katika kutumia zile 4R zake nne anataka twende kwa wananchi tuwaelimishe na wakipende chama chetu, tuwasajili watambulikane kwenye chama chetu na mwisho wa siku tupate ushindi wa Kishindo ambao Rais wetu anautamani" alisema
Mbunge huyo amewasisitiza makatibu wa wilaya zote za mkoa wa Tanga kwenda kutumia vyema nafasi zao kuhakikisha wanaongeza idadi ya wanachama wapya ambapo mpaka kufikia sasa jumuia ya umoja wa wanawake 'UWT' imefikisha wanachama zaidi ya 9052 huku lengo likiwa ni kupata wanachama laki tatu kwa mwaka.
"Sasa katika kutekeleza maelekezo ya Rais na Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa nilileta simu kwaajili ya usajili wa wanachama ndani ya jumuia ya wazazi, vijana na UWT nimewiwa kwasababu tunakwenda kwenye uchaguzi na shauku ya chama chetu ni kuwa na wanachama wengi kuelekea chaguzi zote mbili naamini kupitia jumuia zetu zote ushindi wa chama chetu utapatikana kwa kishindo" alisema Mbunge huyo.
"Kwa sababu shauku ya chama chetu ni kupata mtaji wa wanachama wengi ili kujihakikishia mtaji wa wapiga kura mwaka huu na mwakani naamini ushindi wa chama Cha Mapinduzi ndio utakaonipa uhakika wa mimi kurudi 2025 mshikamano katika jumuia hizi, mashirikiano umoja wetu utahakikisha kwamba tunampatia kura za kutosha Dkt Samia Suluhi Hassan kupigiwa kura kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu"
Kaimu katibu wa umoja wa wazazi mkoa wa Tanga Urassa Kanyaro amempongeza na kumshukuru mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Husna Sekiboko kwa kuwapatia simu hizo ambazo zitakwenda kuamsha na kuongeza ari ya makatibu wa wilaya katika zoezi la usajili ambalo chama hicho limewekeza kuhakikisha tunawapata wanachama wengi zaidi kabla ya uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Alisema kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika hivi karibuni wataungana na UWT pamoja na UVCCM ili kuhakikisha mkoa wa Tanga unashika namba 1 katika Mikoa yote ya Tanzania bara kwenye chaguzi zote.
"Hapo awali zoezi la usajili lilikuwa linasua sua ndani ya mwezi huu tumesajili wanachama 735 na kufikisha idadi ya wanachama 9311ambao ni kati ya wanachama 150,000 wa jumuia ya wazazi kwa kupokea vitendea kazi hivi kutoka kwa mbunge wetu wa viti maalum tutaendelea kutekeleza jukumu hili la usajili kwa kasi na Ari mpya na lengo letu ni kusajili wanachama 700 ndani ya mwezi mmoja kwa kila wilaya" alisema
Akizungumza mara baada ya kupokea simu hizo katibu wa umoja wa vijana 'UVCCM' mkoa wa Tanga amesema Theresia Makiyao amesema mchakato wa usajili wa wanachama wapya kwa upande wao umekuwa ukisuasua kutokana na uchache wa vitendea kazi lakini kupitia Simu hizo itakuwa ni chachu kwao kuzidi kuongeza wanachama wengi zaidi.
"Ukiangalia kwenye takwimu umoja wa vijana tulikuwa tupo chini sana kwenye usaj mpaka kufikia mwisho wa mwezi Mei tulikuwa tumesajili wanachama 994 hii ni kutokana na uchache wa vifaa vya usajili lakini kwa sasa kasi yetu itakwenda juu Sana kwa sababu tayari tumeongezewa nguvu na kasi ya usajili kupitia vifaa hivi ambavyo tumevipoea Leo ila sisi kama umoja wa vijana tutaingia kazini kwa kampeni maalum kuweza kufanya usajili kwa haraka lengo letu kwa Kila wilaya tumejiwekea lazima Kila wilaya iwe imesajili wanachama 500".
Post A Comment: