Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi ameahidi kuchangia shilingi milioni ishirini na tatu kwa ajili ya miradi ya UWT awali amechangia shilingi milioni kumi na moja.

Amesema shilingi milioni kumi atawaanzishia mradi wa kalasha ili kupunguza michango Wanawake.

Katika hatua nyingine ametoa simu mbili na kadi elfu moja kwa ajili ya usajili wa wanachama pia amewataka Wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali zaidi akiwataka Wanawake kushikamana ili kumvusha Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa amefanya mambo mengi ukiwemo ujenzi wa shule, zahanati na miundombinu.

Pia ameahidi kutoa shilingi milioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mpya ya Katibu UWT.

Mbali ya ahadi hizo Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewapatia vitenge kwa ajili ya sare huku akiahidi kukarabati ofisi ya Katibu.
Share To:

Post A Comment: