Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Rajabu Abdulrahman amesema mtumishi yeyote atakayetumia pesa za serikali kwa mambo yake binafsi atazitapika pesa hizo kwani hayupo tayari kumgombanisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassani na wananchi wake.

Rajabu ameyasema hayo mara baada ya mapokezi akiwasili mkoani Tanga akitokea  katika  kikao cha Halmashauri kuu ya CCM  Taifa (NEC) kilichokutana jijini Dar es Salaam na kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa, na kuzungumza na wajumbe wa Halmashauri  ya CCM Wilaya ya Muheza nakusema wapo baadhi viongozi ambao wanatumia pesa za Serikali kwa mambo yao binafsi hivyo hata lifumbia macho suala hilo na mtumishi yeyote atakayetumia pesa hizo kwa mambo yake binafsi atazitapika pesa hizo.

"Hapa Muheza yapo maeneo ambayo Rais ameleta fedha kwaajili ya kujenga kituo cha afya lakini pesa  zilimalizika na kituo cha afya hakijamalizika, hapa muheza wapo mchwa wanaotafuna fedha za Serikali nataka niwaambie mtumishi yeyote atakaye tumia pesa za serikali kwa matumizi binafsi atazitapika zote"- amesema Rajabu.

Katika hatua nyingine Rajabu amechangia kiasi cha shilingi mil10 katika ujenzi wa Jengo la CCM Wilaya ya Muheza na kukabidhi Vifaa vya Ujenzi vilivyotolewa na Viongozi wa Wilaya hiyo ikiwepo mifuko 500 ya Saruji, kokoto,  Mchanga pamoja na tofali.

Nae Mku wa Wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah amesema Halmashauri ya Muheza itaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhudumia wananchi wote bila upendeleo.

Share To:

Post A Comment: