Na Imma Msumba, Arusha

Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi,ccm Mkoa wa Arusha,Rajabu Abdalahman Abdalah ,ambae ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi,ccm,Mkoa wa Tanga,ameagiza Chama Mkoa wa Arusha, kuhakikisha Vikao vya Chama ngazi ya matawi na mashina  vinafanyika  kulingana na ratiba na kalenda ya CCM.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Chama wa ngazi za mashina ,matawi,kata Wilaya  na Mkoa alipokuwa akitambulishwa rasmi kuwa Mlezi wa Chama Mkoa wa Arusha,baada ya kuteuliwa na NEC Juni 30 mwaka huu akijaza nafasi iliyoachwa wazi na marehemu Hassan Mwakasuvi,aliyekuwa Mwenyekiti wa
ccm,Mkoa wa Tabora.
Rajabu,amesema uhai wa Chama ni Vikao kuanzia mashina na matawi huko ndiko kwenye mizizi hivyo lazima vikao vifanyike na wanachama wote bila kujali wadhifa lazima wahudhurie na Vikao hivyo vina uwezo na nguvu ya kumuita na kumhoji kiongozi yeyote aliyekabidhiwa dhama ya Uongozi kwenye ngazi husika .

Amesema ufike wakati wanaopitishwa kugombea Uongozi lazima wawe wanahudhuria Vikao vya mashina na kata kwa kuwa huko ndiko kwenye uhai wa Chama wapo baadhi ya Viongozi huwa hawahudhurii Vikao vya ngazi hizo ambavyo ndivyo muhimu na vimeshikilia hatimae ya uanachama wao.
 
Amesisitiza kwamba  lazima Chama kiisimamie Serikali ili kutekeleza ahadi zilizoko kwenye Ilani ya Chama na kutekeleza Ilani sio jambo la hiari kwa kiongozi au mtumishi wa Serikali bali ni jambo la lazima .

Rajabu,amewataka Viongozi wa Chama kuhakikisha wanaishi kwa kushugulikia changamoto za Wananchi na kuzipatia ufumbuzi na hiyo itawafanya Wananchi wawe na Imani na Chama chao .

Kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu,ametaka  Chama kujipange ili kushinda uchaguzi huo wa Serikali za mitaa,Vijiji,Vitongoji,na Vijiji akahimiza ushirikiano na ameonya Chama kisifanye makosa kitasurubiwa .

Amewataka Viongozi wasitengeneze makundi ya wagombea kwa kufanya hivyo watakuwa wakikigawa Chama wanatakiwa kutambua kuwa wao ni Viongozi na wanakuwa ni kimbilio la kila mgombea Chama kipo kwa masilahi ya umma na sio mtu binafsi .

Amesema kuwa changamoto iliyopo ni kuwepo na Viongozi wa Chama ambao hawana uwezo wa kutafisiri kwa vitendo yaliyomo kwenye Ilani na Katiba  ya CCM .

Kuhusu uchumi amekitaka Chama kuachana na tabia ya kuwa ombaomba hasa wakati wa uchaguzi kwa kutembeza bakuri kwa Wakurugenzi wa halmashauri  badala yake wabuni miradi ya Kiuchumi kwa kutambua kuwa wao ni wasimamizi wa Serikali wakiwa omba omba hawataweza kuwasimamia watumishi pindi wakifanya makosa,wapo Chama kitakuwa na miradi yake ya Kiuchumi kitakuwa kimetengeneza heshima.









Share To:

Post A Comment: