Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewashukuru Wanawake wa Wilaya ya Rungwe kwa kumchagua pia kuahidi kuwa hatawaangusha pia amewataka Wanawake kujikwamua kiuchumi.

"Siasa na uchumi havipishani hivyo ni jukumu la kila mwanamke kujikwamua kiuchumi "amesema Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi huku akiahidi kuvitembelea vikindi vya uzalishaji.

Ameahidi kutoa shilingi 2.5m kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu UWT Wilaya ya Rungwe.

Hata hivyo amewataka Wanawake kushikamana ili kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika ngazi zote na kuwapigani a washinde sanjari na kumuwezesha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ashinde kwa kishindo.

Ametoa simu mbili kwa ajili ya kusajilia wanachama wa UWT Wilaya ya Rungwe lengo ni kupata takwimu nzuri za wanachama.

Aidha amesema mpaka sasa ameiwezesha Wilaya ya Rungwe shilingi milioni kumi na mbili kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kubakiwa deni la milioni nane ili kutimiza ahadi yake ya kutoa shilingi milioni ishirini kwa kila Wilaya.

Hivyo ameahidi kutoa shilingi milioni nne ili kufikia shilingi milioni kumi kwa ajili ya kununua kalasha la kusaga mawe ya dhahabu katika Wilaya ya Chunya ambapo atawaoongezea shilingi milioni nne ambazo watabuni mradi wa maendeleo huku akiishi kauli ya "TWENDE TUKUE PAMOJA".

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Rungwe Twitike Mwalwama mbali ya kumshukuru Mahundi kutoa misaada mbalimbali kwa Wanawake amesema misaada yake imekuwa kichocheo kwani kila Kata hivi sasa wana VICOBA ambapo kila mwaka hugawana na kufanya mambo mengi ya kijamii kama kusomesha.







Share To:

Post A Comment: