Chama cha wafanya kazi wa serikali za mitaa Talgwu Mkoani mara kimelaani tukio la Ofisa mtendaji wa kata ya Nyakonga katika Halmashauri ya wilaya ya Tarime Mkoani Mara ambaye amevamiwa na kukatwa mapanga Nyumbani kwake na watu wasiojulikana.

Akizungumza katika hospital ya rufaa ya kumbukumbu ya mwalim Nyerere Petronia Chiriko Alisema tukio hilo lilitokea Juni 30 mwaka huu amelala yeye na familia yake walisikia kelele ndipo mume wake alipoamka alipochungulia Dirishan waliona watu wakiwa wanavunja Geti la mlango.

" Nilimwambia mume Wangu mbona nasikia kelele tulipochungulia tukaona watu wanavunja geti la mlango nikamwambia mume wangu mbona kama hawa niwezi tumevamiwa tukaanza kupiga kelele ili tupate msaada ili kupiga kelele Ghafla  tukasikia mlio wa bunduki tayari wakawa wamefika mlango wa sebuleni wanavunja kwa shoka"Alisema

 Petroniabaada ya kuingia Ndani walianza kumshanbulia mume Wangu akawa amepoteza fahamu ndio wakarudi kwangu kuanza kuomba pesa kiasi cha shilingi Milioni sita amesema aliendelea kujitetetea kuwa Mume wake ni mwalimu nayeye nimtendaji wa kata fedha zote hizo watazitoa wapi kulikuwa na hela kama laki 7 walisema hawaitaki fedha ile nakuendelea kusisitiza wao wanataka Milioni sita.

Hawakutaka Kabisa kuelewa waliendelea kupekua hadi kwenye mabegi walikutana na laki 4 na 30 fedha za mauzo ya nguo za vitenge lakin waliendelea kusisitiza wanataka Milioni Sita huku wakiwa wananishambulia.

Kutoka na tukio hilo Chama cha wafanya kazi wa serikali za mitaa  tanzania limeviomba vyombo vya dola kuwachukulia hatua kali watakaobainika kuhusika katika tukio hilo.

Aidha Aliopotafutwa kamanda wa polis Tarime Rorya simu yake iliita bila majibu

Share To:

Post A Comment: