Na Ashrack Miraji Kilimanjaro 

Singa, Kilimanjaro Mwenyekiti wa kitongoji cha Singa kifueni Joseph Ngowi, na Mwenyekiti wa kitongoji Cha Singa juu Raphael Malliya wametoa taarifa kuhusu huduma zinazotolewa katika Zahanati ya Matella kwamba imekuwa msaada mkubwa kijijini hapo.


Akizungumza na mwandishi wetu, Joseph Ngowi alisema kuwa zahanati hiyo imekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Kijiji cha Singa na vijiji jirani katika Kata ya Kibosho.


"Zahanati ya Matella inatoa huduma bora kama vile vituo vya afya vya serikali, lakini kwa gharama nafuu ambazo kila mwanakijiji anaweza kumudu. Wananchi wamefurahishwa na ubora wa huduma na jitihada za mfadhili Joseph Mushi katika kujenga zahanat hiyo."

Mwenyekiti aliongeza kuwa wananchi wa vijiji vya mbali na wageni wanapata huduma bila wasiwasi, kwani zahanat imejengwa kwa lengo la kuhakikisha kila mtu anapata huduma nzuri kwa gharama nafuu. Wananchi wanaweza kutibiwa Kwa gharama nafuu sana, za kuchangia umeme, maji, na Dawa bila kikwazo.

Grace Peter, mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Singa, alishukuru kwa huduma nzuri wanayopata katika zahanati hiyo. Madaktari wanatoa huduma kwa kiwango kikubwa, na zahanati imekuwa mkombozi kwa wakazi wa Singa.


 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: