Vijana nchini wametakiwa kutumia kwa usahihi mitandao ya kijamii kwa manufaa yao binafisi pamoja na kueleza mema na mambo mazuri ambayo yameendelea kufanywa na serikali ya awamu ya sita na kuepukana na vitendo vya uchonganishi pamoja na matumizi yasiyo sahihi ya mitandao hiyo

Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) Rehema Sombi  wakati akizundua kambi la mafunzo ya vijana wa CCM Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita.

Amesema mitandao inaweza kuwa na tija na faida kubwa ya kiuchumi kwa vijana endapo kama itatumika vizuri.

“Kwasasa sayansi na teknolojia imeboreshwa kwa kiasi kikubwa tunajua kuna vijana wanatumia mitandao ya kijamii kama ajira,lakini pia kumekuwepo na waathirika wakubwa wa mitandao ya kijamii wamekuwa ni vijana tunatakiwa sasa vijana tubadilike na kutumia mitandao hii kama sehemu ya kukuza vipato na kutengeneza uchumi imara”Amesema Rehema Sombi.

Sombi ameongeza kuwa uwepo wa kambi za mafunzo za vijana wa CCM zimekuwa na tija kutokana na namna bora ambayo vijana wamekuwa wakifundishwa mbinu mbalimbali zikiwemo za kujijenga kiuchumi lakini pia kujua Historia ya chama pamoja na suala la maadili.

Sanjali na hayo Sombi amewahimiza vijana kutumia fursa za mikopo inayotolewa kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri  kwa kuendesha miradi mbalimbali  ambayo watabuni na kuamua kuianzisha.

Share To:

JOEL MADUKA

Post A Comment: