MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma ,Fatma Toufiq (CCM) amekabidhi mitungi 200 ya gesi aina ya Oryx kwa wajasiriamali wanawake Wilaya ya Chemba. 

 Akizungumza leo June 11,2024 Wilayani Chamwino mara baada ya kuwakabidhi,Mbunge huyo amesema kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi kutumia gesi na nishati mbadala na kuacha kutumia mkaa na kuni ili kuepukana na uharibifu wa mazingira nchini na anamini mitungi hiyo itaendelea kulinda ndoa kwani kina mama watatumia muda mchache kupika chakula na kutotembea umbali mrefu kusaka kuni na mkaa.

 "Tunaendelea kumuunga mkono Rais Samia katika matumizi ya nishati safi Mimi kama Mbunge wenu nitaendelea kupiga hodi katika maeneo mbalimbali ili lengo la asilimia 80 kutumia nishati hiyo liweze kufikiwa"

 Kwa upande wake,Meneja Mauzo Kanda ya kati kampuni ya Oryx,Jeniffer Mosha amesema wanaunga mkono jitihada za serikali katika suala la utunzaji wa mazingira na anaamini kupitia mitungi hiyo wananchi watatunza mazingira.

Baadhi ya akina mama lishe wamempongeza Rais Dkt Samia Suluhu na Mbunge toufiq  kwa kuwawezesha kupata majiko hayo na kuhaidi kuwa mabalozi wazuri katika kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira hasa ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa pamoja na kuni kwa ajili ya kupikia na badala yake watu watumie nishati mbadala ikiwemo gesi.

Share To:

Post A Comment: