Na Carlos Claudio, Dodoma.


WAKALA wa wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) limejikita katika kutoa huduma na elimu kupitia mifumo ya kidijitali nchini, kuelekea wiki ya maadhimisho ya utumishi wa umma 2024 imeweza kufikia wafanya biashara nchini na kutoa elimu ya mifumo itakayowasaidia wafanyabiashara kupata huduma kwa urahisi. 


Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 20, 2024 jijini Dodoma, Afisa utumishi mkuu Migisha Kahangwa amesema wiki ya utumishi wa umma ni tukio ambalo lipo katika kalenda ya umoja wa Afrika ambapo wanachama hushiriki kuonyesha huduma mbali mbali zinazotolewa na utumishi wa umma.


Amesema BRELA kama moja ya taasisi ya umma katika wiki ya maadhimisho imekuja kuonyesha na kutoa huduma zake kwa wananchi wa ndani na nje ya mkoa wa Dodoma.


“Brella inakuzisha biashara kwa kusajili makampuni , majina ya biashara, alama za huduma na biashara, kutoa leseni za viwanda pamoja na kutoa leseni za biashara daraja `A’ ,”


“Tunawakaribisha wananchi wa mkoa wa Dodoma pamoja na mikoa ya jirani na vitengo vyake waweze kushiriki kwasababu tunatoa huduma moja kwa moja mahali hapa ambapo kila mwananchi anauefika anapata huduma moja kwa moja na kuondoka pamoja na cheti chake.” amesema Migisha Kahangwa.


Amesisitiza wananchi kutumia vyema mifumo ya TEHAMA ili waweze kusajili huduma zao ili wafanye biashara zao kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa na nchi.


Kwa upande wake afisa usajili kutoka wakala wa usajili leseni BRELA Gabriel Girangay amesema BRELA kama taasisi ya umma ambayo kazi yake ni kusajili makampuni, majina ya biashara, alama za biashara na huduma, kutoa leseni ya viwanda,


Amesema BRELA imekuja katika viwanja vya Chinangali ili kuhakikisha wadau pamoja na watumishi wa umma wanaojihusisha na biashara wanasaidiwa kutokana na  matatizo ambayo wanakutana nayo katika usajili na shughuli zingine za biashara.


Girangay amesema kuwa wamekuwa wakitembelea wafanyabiashara katika maeneo yao ili kutatua changamoto mbali mbali ikiwemo ya elimu juu ya mifumo yao kwani huduma zote zinatolewa kwa njia ya mifumo.


“Kwa sasahivi tunafanya shughuli zetu bila kutumia makaratasi, tunatumia mfumo wa kompyuta kwa upande wa BRELA inaitwa ORS (Online Registration System)  ambayo utatumia katika kupata huduma zote za BRELLA ikiwa ni pamoja na kupata taarifa yoyote ya kampuni unayohitaji nchini,”


Giangay ameongeza kuwa, “sheria inamuhitaji kila mfanya biashara ajirasimishe kwasababu ukirasimisha biashara yako unapata faida nyingi ikiwa pamoja na uwezo wa kupata huduma za kibenki, kupata tenda mbali mbali za serikali na sekta binafsi lakini pia kupata ubia kwasababu watu wengine kutoka nje ya nchi wakifika nchini hawaangaiki kusajili kampuni wanachofanya wanawatafuta watu ambao teyari wapo sokoni wanafanya biashara hivyo wanaungana nao.”


Aidha amesisitiza makampuni pamoja na majina ya biashara kuwa na tabia ya kutoa taarifa kila ifikapo mwaka kupitia fomu na 128 ili BRELA iijulishe mtu yoyote anayehitaji taarifa za kampuni kuwa ipo sokoni na inafanya biashara.






Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: