Afisa Masoko kutoka chuo Cha Sayansi ya Afya Korandoto Shinyanga Josephine Charles akizungumza na Waandiahi wa habari katika maonyesho ya Elimu u unifu na ujuzi yanayoendelea kufanyika kitaifa mkoani Tanga katika viwanja vya Popatlal.


Na Denis Chambi, Tanga.

SERIKALI imeombwa kuangalia namna ya kuweza kuwasaidia  wanafunzi wanaosomea taaluma mbalimbali kwenye ngazi ya vyuo vya kati hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuwapatia mikopo  ya elimu ili iweze kuwasaidia kutimiza ndoto zao pamoja na kuwajengea uwezo  hatua mabyo itaiwezesha kuongeza nguvu kazi ya Taifa katika kutoa huduma kwa jamii.

Ombi hilo limetolewa na mkuu wa chuo cha Sayansi za afya 'Korandoto' kilichopo mkoani Shinyanga Paschal Shiruka wakati akizungumza katika maonyesho ya elimu ubunifu na ujuzi yanayofanyika kitaifa mkoani Tanga ambapo amebainisha kuwa wimbi kuwa la wanafunzi wanajiunga na vyuo vya elimu hapa nchini wamekuwa walishindwa kumaliza masomo yao kutokana na kukosa fedha hali inayopelekea kushindwa kufikia ndoto zao.

Amesema Kupitia bodi ya mikopo ' HESLB' ambayo unawapa mikopo wanafunzi wa elimu ya juu waliopo kwenye vyuo mbalimbali hapa nchini ni vyema kuwatazama na wanaosomea vyuo vya kati ili kuongeza wataalam wengi zaidi katika kada mbalimbali jambo ambalo pia litaisaidia Serikali kupata nguvu kazi  na hatimaye kuongeza utoaji huduma kwawananchi.

"Haya mafunzo ya kati kwa sababu ndio wanahitajika  zaidi kwenye jamii basi tunaomba waendelee kusaidiwa maana wanatoka wengi kwenye familia zile ambazo  hazina uwezo hii ikifanyika itasaidia kupata watumishi wengi lakini kuwapunguzia gharama ambapo wataweza kusoma na kuhitimu mafunzo"

"Hawa wanafunzi wa vyuo vya kati tunatamani waingizwe kwenye mfumo wa mikopo wa kuwa  ndio wengi zaidi ninaamini hata bodi ya mikopo itanufaika zaidi kuliko kwenye vyuo vikuu na hawa ndio wanahitajika kwa wingi tunaamini wakikopeshwa  hata kule kurudisha ile mikopo itakuwa ni rahisi zaidi kwa sababu kwenye ajira ndio wanaopatikana wengi takwimu zinatuonesha kwamba wanajiunga wengi lakini wengi wao wanaishia njiani  tunaona sasa nguvu kazi ya nchi ambayo ilikuwa ipatikane inapotea bure" alisema Shiruka.

Aidha Shiruka amesema kuwa vyuo vingi hapa nchini  hususani vyinavyotoa taaluma ya afya vimekuwa vikishindwa kujiendesha kwa ufanisi kutokana na gharama kuwa kubwa pamoja na wataalam jambo ambalo ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuzisaidia taasisi ambazo ni za binafsi.

"Changamoto kubwa sana kwenye mafunzo haya ya afya  huwa ni gharama za uendeshaji   na ndio hii inayopandiaha gharama kwa wanafunzi kujiunga na mafunzo, katika jamii wanafunzi wako wengi lakini wanashindwa kujiunga na vyo kwa sababu ya gharama  kubwa "

Ombi hilo linakuja kufwatia kauli ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda  wakati akifungua maonyesho hayo  hivi karibuni ambapo amesema kuwa Serikali inaendelea kuwapa kipaumbele wanafunzi  wanaosoma masomo ya Sayansi ambapo baada ya kumaliza kidato cha sita na kufanya vizuri kwenye mitihani yao watagharamikiwa kwa asilimia 100 kusoma bure  vyuoni mpaka watakapomaliza.

"Tumeanzisha elimu kupitia Skolarship ya Samia Sasa Kama wewe ni mwanafunzi na unasoma masomo ya Sayansi  kati ya wanafunzi bora 600-700 watakaomaliza kidato cha sita na kuamua  kusoma vyuo vya ndani wanafunzi hao watalipiwa gharama zote na Serikali kwa asilimia 100  gharama zote pamoja na za kujikimu mpaka watakapomaliza  masomo yao"

Akizungumza afisa Masoko wa chuo hicho Josephine Charles ameipongeza Serikali kutokana na kuboresha maonyesho hayo Kila mwaka jambo ambalo kimekuwa likileta ushindani miongoni mwa washiriki katika utoaji wa huduma kwa jamii.

Amesema ushiriki wao katika maonyesho hayo yanayovihusisha vyuo vya elimu ujuzi na ubunifu hapa nchini  yamekuwa na tija ndani ya chuo hicho cha Kolandoto baada ya mwaka 2023 kuibuka kidedea na kuwa mshindi wa  tatu  kwa taasisi zilizofanya vizuri.

"Maonyesho ya mwaka huu ni makubwa  tofauti na miaka ya nyuma kwetu sisi inatusaidia kutujenga na kututangaza zaidi kwa sababu tunakutana na Watu wengi lakini inatupa changamoto sisi vyup vya kati kutamani kwenda vyuo vikuu, tunatoa fursa za ajira kwa wanafunzi wanaofanya vizuri kitaaluma ndani ya chuo chetu na hii inatupa mwanya wa sisi  kuweza kuisaidia jamii"


Mkuu wa chuo cha Sayansi za afya 'Korandoto' kilichopo mkoani Shinyanga Paschal Shiruka  akizungumza na Waandishi  wa habari katika maonyesho ya Elimu ujuzi na ubunifu yanayofanyika katika viwanja vya Popatlal Mkoani Tanga.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda  akitembelea mabada  ya washiriki kutoka vyuo na vyuo vikuu  vilivyoshiriki katika maonyesho ya elimu ujuzi na ubunifu wakati alipoyafungua rasmi Mey 27 mkoani Tanga.


Share To:

JOEL MADUKA

Post A Comment: