SERIKALI itaendelea kuwatambua wabunifu nchini  kwa lengo la kuchagiza maendeleo ya uchumi na kijamii sanjari na kubiasharisha teknolojia na bunifu ili kukuza uchumi kwakutumia teknolojia zinazoibuliwa sanjari na kuzilinda.

Akizungumza kabla ya uzinduzi wa Uanzishwaji wa Madawati na jukwaa la Sayansi, Teknolojia na UbunifuNaibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Dk,Franklin Rwezimula amesema kwa Sasa serikali imeendelea kuhakikisha bunifu zinakuzwa ambapo bunifu 283  zilibuniwa na watanzania ,huku bunifu 42 kati ya hizo zimeingia sokoni

"kwa ulimwengu tunaoishi huwezi kuikwepa sayansi na teknolojia  ila tunachotakiwa kufanya ni kuwatambua wabunifu sehemu walipo kwa kuwafikia na kuendeleza ubunifu wao kwasababu serikali imetenga fedha kwaajili yakutekeleza ubunifu katika nyanja mbalimbali na mpaka sasa tumegundua bunifu zaidi ya 283 zilizobuniwa na watanzania huku bunifu 42 zikiwa zimeshaingia sokoni,kwa kupitia mahusiano hayo kutaongeza chachu ya ubunifu katika maeneo tofauti ya nchi yetu."alisema

Dkt.Franklin   amebainisha uwepo wa madawati na majukwaa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yatawezesha bunifu zinazoibuliwa kutambulika ikiwemo bunifu mpya zinazozalishwa katika kata,wilaya na mikoa mbalimbali na kupata fursa za kuongezewa ujuzi zaidi na serikali .

Naye mkurugenzi,Idara ya Sayansi,teknolojia na ubunifu (DSTI),WyEST amesema mafunzo haya wizara iliandaa na kuridhia kwa uanzishwaji wa madawati ya majukwaa katika shule za msingi na sekondari ikiwa na lengo kuu la kuhakikisha kwamba wanaendelea kuimarsha utaratibu na uhamasishaji wa maswala ya sayansi na ubunifu kwasababu ni sehemu ya maisha yetu kila mahali na kwa kila ngazi hivo jamii kupata uelewa wakutosha na si tu kushiriki kama wagunduzi bali  kushiriki kwa kuhakikisha kwamba wanatumia mazao hayo  ya sayansi,teknolojia na ubunifu katika mizunguko ya ya maisha

Sambamba na hilo mshiriki wa mafunzo Abubakari Hussein amesema kuwa mafunzo haya yatawasaidia na watayafanyia kazi na kwa mkoa wa Arusha watafanya vizuri kama maelekezo yalivyotolewa na kuwafikia wabunifu wa aina zote watapatikana na yale malengo ya serikali  yaliyokusudiwa yatafanyiwa kazi.












Share To:

Post A Comment: