Na Ashrack Miraji Same Kilimanjaro 

Mwenyekiti wa kitongoji Cha Singa Juu,Ignas Mallya ameyasema hayo wakati akiongoza  kikao cha wananchi kwa lengo la kuwachagua   wawakilisha watatu watakao  wawakilishi kwenye kamati mpya ya bodi ya  maji katika kijiji hicho  chenye  vitongoji vinne Singa Chini ,Kati, Kifueni,na Singa Juu vya Kata ya Kibosho wilayani Moshi  Mkoani Kilimanjaro.

"Niiombe  Serikali iweze kutusaidia sisi wananchi wa  kijiji Cha Singa kuhusu suala la Maji katika kijiji chetu,tumekuwa na changamoto kubwa hasa katika kulipia maji ambayo yanatokana na nguvu kazi zetu  kuanzisha chanzo cha maji kwenye Kijiji chetu.Kuna watu wengi wamepoteza maisha na wengine kutoa ardhi zao ili maji yaweze kupita bila ya kulipwa fidia yoyote hadi sasa"

Huduma ya maji ni huduma ya kila mwananchi hivyo tulikuwa tunaiomba serikali kutokana na nyakati za sasa kuazishwa  bodi za maji kupitia Halmashauri kuwa na  jukumu ziweze kusimamia huduma za maji vijijini,basi kijiji chetu kiwe na Kamati ambayo inasimamia maji na kuingiza mapato kwenye  Kijiji chetu.Nimeteseka kipindi kirefu maana tulikuwa na kamati ya maji hapa kijijini ambayo ilikuwa haifanyi kazi Kwa wakati na kusikiliza kero za wananchi hususani kwenye huduma ya maji" amesema Ignas Mallya.

Mwenyekiti Mallya aliendelea kusema "nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipo washukuru wadau wa maendeleo hasa kijana wetu,Joseph Mushi amekuwa mtu wa watu mpenda maendeleo katika kijiji hiki na kutusaidia mambo  mbalimbali ya kiuchumi na kututaka pia tuchague kamati makini ya maji, itakuwa chachu ya maendeleo katika Kijiji chetu na kutatua matatizo na kusimamia huduma ya maji hapa Singa"

Kikao hicho kimechagua wajumbe watatu katika vitongoji vinne il kwenda kuungana na vitongoji vingine ambao wapo kwenye kijiji hicho kupata wajumbe tisa watawawakilisha wananchi kwenye bodi ya maji ambayo imeudwa na serikali (Sikika) lengo pia ni kutaka kuishauri Serikali juu ya  usimamizi wa maji katika kijiji chetu.




 
Share To:

ASHRACK

Post A Comment: