Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka amegawa mipira 1000 kwa shule za Msingi Mkoa Mzima wa Njombe na kuwaagiza Maafisa Michezo wa Halmashauri zote wakiongozwa na Afisa Michezo Mkoa wa Njombe Kuhakikisha Wanaandaa Utaratibu Mzuri wa Watoto Kucheza Mpira wa Miguu Wawapo Shuleni au Kipindi cha likizo ili Kuwajengea Afya bora na Kukuza Vipaji Vyao.

Akizungumza na Viongozi wa Chama cha Soka Mkoa wa Njombe, Maafisa Michezo na Walimu wa Michezo katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Njombe (NJOSS) Aprili 23 /2024, Mhe. Anthony Mtaka amesema wao kama Taifa wanaiangalia Michezo kama Fursa ya kuwatengeneza Matajiri kama ilivyo kwa wachezaji wanaotazamwa Nchini kama Mbwana Ally Samatta na Wengine.

Mhe. Mtaka amesema, "Wazazi wanao wajibu wakuwaangalia watoto wao katika Michezo kama ambavyo wanawaangalia katika Elimu."

Share To:

Post A Comment: