1000675603


Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. LAZARO BUSAGALA ambaye pia ni Mratibu wa Kitaifa wa Zoezi la Utayari dhidi ya dharura za kikemikali na kimionzi Tanzania (ZOKIKITA 2024) amesema TAEC itahakikisha inaendelea kushirikiana na wadau muhimu katika zoezi hilo ili kutekeleza maelekezo ya Waziri Mkuu Mh. KASSIM MAJALIWA hususani kupeleka elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa ZOKIKITA.

Prof. BUSAGALA ameyasema hayo jijini Dar es salaam ambapo amesisitiza kuwa maelekezo ya Mh. Waziri Mkuu ya kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya namna ya kujilinda dhidi ya dharura za kikemikali na kimionzi yanatekelezwa kwa vitendo na elimu itatolewa kwa njia za redio, tv, magazeti na mitandao ya kijamii.

Wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa kukabiliana na dharura za kikemikali na kimionzi Tanzania Jijini Dar es salaam .

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa alielekeza elimu itolewe kwa wananchi kupitia vyombo vya Habari ili wananchi wafahamu namna ya kukabiliana na dharura za kikemikali na kimionzi kazi ambayo wadau wa maeneo hayo wameanza kuitekeleza kwa vitendo kwa kupita katika vyombo vya habari kutoa elimu.

Kwa upande wake Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania DCP DAVID MISIME amesema jeshi la polisi litaendelea kushirikiana na Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania pamoja na taasisi zingine ili kuhakikisha utayari unakuwepo katika kukabiliana na majanga.
Share To:

Post A Comment: