Na Denis Chambi, Tanga.

WIZARA ya Afya kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imetenga kiasi cha Shilingi Trilion 2.4 sawa na asilimia 8 ya bajeti kuu ya serikali kwaajili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ambayo ni pamoja na Kipindupindu.

Hayo yamebainishwa na mchumi idara ya sera na mipango kutoka wizara ya afya France Lasway wakati wakitoa semina kwa waandishi wa Habari iliyofanyika kwa njia ya mtandao ambayo iliandaliwa na Chama cha waandishi wa Habari Wanawake Tanzania ‘TAMWA’ ambapo katika bajeti hiyo wizara ya afya inakadiriwa kuwa na kiasi cha asilimia 7.3 kimetengwa kwaajili ya utayari wa kukabiliana na magonjwa hayo.

Amesema kuwa wizara imesimamia uanzishwaji wa vituo viwili vya oparesheni ya matukio ya dharura (PHEOCs) katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha hivyo kufikia idadi ya vituo 6 pamoja na kutoa mafunzo maalumu kwa wataalam wa vituo hivyo.

Aidha katika utayari, udhibiti na kukabiliana na magonjwa hatari ya kuambukiza na mlipuko wizara ya afya kwa kushirikiana na TAMISEMI pamoja na wizara ya maji imezindua mpango shirikishi wa Taifa wa kukabiliana na Kipindupindu kwa kipindi cha mwaka 2023 hafi 2027 ikiwa na lengo la ushirikiano wa sekta mbalimbali katika kukabiliana na janga la Uviko-19 ambalo limeathiri nchi nyingi Duniani.

Ameendelea kwa kusema wizara imeendelea kukabiliana na ugonjwa huo ikiwemo kuimarisha upatikanaji wa hewa tiba ya Oksjeni kwa kusimika mitambo 19 ya kuzalisha Oksjeni katika Hospitali za Rufaa, mikoa.

Mikoa hiyo iliyoguswa na mpango huo ni Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara, Mbeya, Dodoma, Geita, Manyara, Mwanza , Kigoma , Katavi, Ruvuma, Kigoma, Katavi, Songwe, Lindi, Morogoro, Njombe, Simiyu, Mara, Tabora, Rukwa na Shinyanga.

“Mitambo mingine ipo katika hatua za manunuzi ambapo inatarajiwa kusimikwa pindi itakapowasili na kufanya mitambo ya Oksjeni kufikia 55 katika ngazi za Taifa, Kanda, Mikoa, na wilaya nchi nzima” alisema.

Hata hivyo wizara hiyo inaratibu na kutekeleza afua za elimu ya afya na ushirikishaji wa jamii kuhusu dharura mbalimbali za afya ikiwemo madhara ya kiafya yanayoweza kujitokeza kutokana na tishio la mvua za Elnino na mafuriko.

Kwa upande wake Richard Msittu kutoka shirika la Sikika amesisitiza umuhimu wa jamii kuzingatia usafi wa maeneo yanayowazunguka ikiwa ni pamoja na kuwa na vyoo safi na salama sambamba na kutoa elimu kwa lengo la kuongeza uelew kwa wananchi wa jinsi ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ambayo yamekuwa yasababisha athari mbalimbali.

“Suala la kuzingatia usafi katika mazingira ya binadamu ikiwemo katika masoko tunaponunulia na kuuzia vitu hii itasaidia sana lakini pia kutoa elimu jamii ili kuongeza uelewa kwa jamii katika kuzuia magonjwa hayo” alisema.

Alisema wizara kwa kutambua umuhimu wa utayari wa kukabiliana na na mahonjwa ya mlipuko na ya kuambukiza wizara ya afya itaendelea kutekeleza vipaumbele mbalimbali ambavyo ni pamoja na kuimarisha huduma za kinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza ikiwemo chanjo ya elimu ya afya kwa Umma kwa kuimarisha huduma za dharura na ajali nje na ndani ya Hospitali.

“Katika kuimarisha huduma za kinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza katika kuteng bajeti ambako kutasaidia utayari kwa kuwepo wataalam, vifaa tiba, vitendanishi na miundombinu, kutoa elimu ya afya kwa Umma za ngazi ya jamii kujikinga na athari za magonjwa ya mlipuko” alisema.

Aidha kufwatia Ugonjwa wa macho (Red Eyes) ambao umesambaa katika mikoa mbalimbali wananchi walioathirika wametakiwa kwenda katika vituo vya afya ili kupata matibabu na sii vinginevyo ambapo vipimo vitaweza kubainisha sababubj na kupata matibabu ya haraka.

Share To:

Post A Comment: