NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Dkt Festo Dugange amesema katika kipindi cha mwaka 2022 hadi 2023 jumla ya Wajawazito 10,829 walipewa vifaa vya kujifungulia katika vituo vya huduma ya afya ya msingi na kuwawezesha kupata huduma hiyo.

Mhe Dkt Dugange ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe Anatropia Theonest aliyehoji idadi ya wanawake walioshindwa kumudu ‘delivery kit’ na kupewa vifaa hivyo na Hospitali au Kituo cha Afya husika.

“ Serikali inaendelea kutoa huduma za afya kwa wajawazito wanaojifungua kwa kuzingatia sera ya afya ya mwaka 2007. Sera hii imeainisha makundi ya matibabu kwa msamaha ikiwemo huduma ya wajawazito na kujifungua. Katika kipindi cha mwaka 2022 na 2023 juml ya wakina Mama 2,707,098 walijifungua kwenye vituo vya kutolea huduma ngazi ya msingi.

Moja ya huduma inayotolewa katika vituo ni kitita cha kujifungulia (delivery kit) kwa wajawazito wasiomudu ambapo jumla ya wajawazito 10,829 walipatiwa vifaa hivyo,” Amesema Mhe Dkt Dugange.

Share To:

Post A Comment: